Askari wa kikoloni wakifaransa waliwaua Waafrika wengi kwa lengo la kukusanya fuvu zao ili kuimarisha Makumbusho yao ya historia (Museums) na walikuwa wakiingiza fedha nyingi sana kwenye hayo makumbusho yao. Na walienda mbali zaidi kwa kuweka picha za vichwa vya waafrika kwenye Stempu Zao kwa ajili ya kutuma Barua. Historia hii haitasahaulika, kwa vizazi hadi vizazi.
Mleta mada hii huwezi kupata wachangiaji umeharibu kusema mkoloni mfaransa.
Ungesema mkoloni mwarabu sasa hivi bandiko lako lingesha sheheni wachangiaji mpaka ungesikia raha..
Lakini unawasema wafaransa wazungu umebugi mkuu.
Dhambi walizotufanyia hao wakoloni wazungu hazitasameheka na wametengeneza wakoloni weusi wanatutawala mpaka leo jamaani tupiganie ukombozi wetu na wa mtu mweusi