Geza Ulole
JF-Expert Member
- Oct 31, 2009
- 65,136
- 91,917
Askari wa kikosi maalum cha Uingereza aokoa watu shambulio la kigaidi Kenya
THURSDAY JANUARY 17 2019
Kwa ufupi
Shambulizi hilo lilianza kwa mlipuko uliofuatiwa na milio ya risasi katika hoteli ya Dusit katika eneo la Chiromo, mjini Nairobi
Mtu aliyeonekana kuwa na silaha nyingi ambaye alikuwa akishirkiana na vikosi vya Kenya na akisaidia katika kuokoa watu jijini Nairobi katika shambulio la kigaidi, alikuwa katika kikosi maalum cha Uingereza, vyombo vya habari viliripoti jana.
"Bila mwanajeshi huyu wa kikosi maalum cha Uingereza, maisha ya watu wengi zaidi yangepotea," limeandika gazeti la Daily Mirror likimkariri mtu kutoka jeshi la uingereza.
"Vitendo vyake visivyo vya kibinafsi vitakumbukwa na wale aliowakoa na pia atasifiwa na wanajeshi wenzake," alisema mtu huyo.
Gazeti hilo limesema askari huyo alikuwa sehemu ya timu ndogo "ya pamoja" iliyounganishwa kwenye vikosi maalum vya Kenya.
Mwanajeshi wa zamani wa vikosi hivyo maalum, Chris Ryan alikaririwa na gazeti hilo akisema mtu huyo alikuwa akifanya manunuzi wakati shambulio hilo lilipoanza.
Gazeti la The Times lilisema ni "mtumishi wa muda mrefu" wa kitengo cha Uingereza cha wanajeshi bora cha anga kinachoitwa Huduma Maalum za Anga au SAS (Special Air Service).
Picha za mtu huyo, aliyekuwa amevalia jeans na kujifunika uso, zinaonyesha akiokoa watu katika tukio hilo. Alivaa nusu koti la kubebea silaha ikiwa na bunduki mgongoni na bastola mkononi.
Kwa kawaida serikali ya Uingereza haizungumzii masuala ya vikosi maalum.
Askari watano wa kikundi cha Al-shaabab cha Somalia ambacho kina uhusiano na kundi la Al-Qaeda-, walishambulia hoteli ya DusitD2 na jengo la ofisi jijini Nairobi Jumanne na kuua watu wapatao 21.
Askari wa kikosi maalum cha Uingereza aokoa watu shambulio la