Askari wa Kituo cha Polisi Mabwepande wadaiwa kuwapora vijana wa bodaboda pesa

Askari wa Kituo cha Polisi Mabwepande wadaiwa kuwapora vijana wa bodaboda pesa

Pdidy

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2007
Posts
57,951
Reaction score
32,619
Nilichokiona jana na leo hapa Boko Magengeni ni aibu kabisa.

Askari walikuja na defender wakashuka na kuwavamia vijana waliopaki pikipiki zao za biashara. Mara tukasikia wanauliza “we una sh. ngapi??” Abiria wote tuliokuwa pale tulishangaa.

Yaani inashangaza, hadi buku 3 askari anachukua. Kama hamuamini kawaulizeni wale vijana! Wengine wakawa wanasema “ndio kwanza tunaanza kazi afande” lakini hawakuwaelewa.

Uongozi wa Jeshi la Polisi saidieni wale vijana, hawaingizi mamilioni wala bali wanatafuta elfu kumi kumi wakale na familia zao.

Mungu awabariki na ni matumaini yangu wataonywa.
 
Awamu pendwa hii...kila kitu ruksa umesahau mmakunduchi sawa na Mwinyi era...ruksa
 
Back
Top Bottom