Askari waliokimbia mapigano DRC kupandishwa kizimbami leo

Askari waliokimbia mapigano DRC kupandishwa kizimbami leo

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Wanajeshi 75 wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) wanapandishwa kizimbani leo Februari 10, 2025 wakituhumiwa kukimbia mapigano baina ya vikosi vya Serikali na waasi wa M23.

Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Mwendesha Mashtaka ya Kijeshi wa DRC imeeleza kuwa askari hao pia wanashtakiwa kwa tuhuma za kufanya vurugu dhidi ya raia ikiwa ni pamoja na mauaji na uporaji.

1739170808449.png
"Wanajeshi 75 wanaokabiliwa na kesi walikamatwa kwa kukimbia mapigano baada ya kushikiliwa kwa Mji wa Nyabibwe. Wanatuhumiwa kwa ubakaji, mauaji, uporaji na uasi,". imeeleza taarifa hiyo

Umoja wa Mataifa umeripoti kuwepo kwa vitendo kadhaa vikiwemo ya unyongaji, ubakaji wa magenge na utumwa wa kingono hasa katika eneo la Mashariki la Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.

Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa imedai kuwa waasi wa M23 na askari wa Serikali ya DRC pamoja na wanamgambo wanaoiunga mkono Serikali wote wanahusika.

Soma, Pia:
 
Hii inakkata motisha kabisa kwa askari wa kongo ndo maana wengi wanaona bora kuasi
 
Kila nikisoma nyuzi na comments za wabongo zinazohusu M23 na Rwanda kisha niitafute hiyo Rwanda kwenye ramani kalivyo kadogo naishia kuchoka sana.
 
Sasa kuna umuhimu gani kwa nchi zingine kupeleka majeshi yao kama jeshi mwenyeji linakimbia mbele ya adui. Tena wewe umepunguza idadi au kwamba wanashitakiwa kwa mafungu. Taarifa ya BBCswahili inasema "MAELFU ya wanajeshi wa Congo kushtakiwa kwa KUWAKIMBIA waasi wa m23"
 
Drc haina jeshi ila ina mkusanyiko wa wanamgambo wa kikabila
Tishekedi alikuwa anawalipa wale Mamluki wa Kiromania dola 4000/5000 kwa mwezi halafu hawa Askri wa Kikongo wanalipwa 100$ na mara nyingine hata huwa hawapokei.

Halafu hata mabomu ya kwenye Vifaru pia pesa zinapigwa unakuta Kifaru kizima kina makombora mawili au matatu na mafuta yenyewe wanapewa kiduchu.

Sasa unataka hawa Askari wapigane vipi?!
 
Ndio Bata Eleza mahakama ya Kijesh!!!
 
Kama juz karibia battalion nzima imekimbia mapigano tena imekimbilia kwa adui yao ambae n Rwanda
 
Back
Top Bottom