Askofu anamiliki HAMMER ya 250million!

Status
Not open for further replies.

Makubwa! utacagua msaada? alafu bandarini kwanini hawaukuizuia? sasa huyu pastor asiye na elimu ya mazingira anajua wapi jamani? mumfate mmwambie sidhani kama atakataa badala ya kwenda kwa Shigongo of all papers for a pastor to read!
 
Kumiliki hammer au vitu vya thamani kwa viongozi wa dini si dhambi kama walivipata kiuhalali! Mbona mtume suleimani alikuwa na mali nyingi tu na hakuwa dhambi, dhambi ni jinsi avitumiavyo kwa ajili ya anasa, kama anavitumia kwa shughuli za MUNGU basi na ataongezewa sana
 

Unanishangaza! Kwa hiyo watu masikini hawataweza kushiriki katika kanisa hilo maana hawatakuwa na uwezo wa kutoa sadaka nyingi? Na ni mazuzu wanaodanganywa na wasio na uelewa? Kwa hiyo huyo Mungu wenu tajiri SI Mungu wa watu masikini wamwombao kila kukicha? Hao watu matajiri wanaojidai wanatoa hela nyingi ndio wanafiki wakubwa na ndio ambao Yesu aliwaita "Mafarisayo wanafiki mnaoosha vikombe kwa nje wakati ndani kumejaa uvundo" na mama aliyetoa pini ndiye aliyetoa kikubwa zaidi. Wewe kama Askofu unayeongoza kundi la Muumba kwa nini uwe na gari expensive kiasi hicho wakati kuna watu wengi ambao wangenufaika sana na hiyo 30,000 ambayo kwako haiwezi hata kuwasha gari lako?
 
Unanishangaza! Kwa hiyo watu masikini hawataweza kushiriki katika kanisa hilo maana hawatakuwa na uwezo wa kutoa sadaka nyingi?
Sijawahi kusikia hivyo ndo unaniambia wewe, na je we unayehoji matumizi yao: wewe gari lako unapkia maskini wangapi? unaishi na wsiojiweza na yatima wangapi? UNASEMA HABARI YA YESU, je lini uliacha vipindi vya TV, overtime zako, likizo ukaenda kuomba watu wampokee? watu waache dhambi? kuwahudumia wagonjwa usiowajua? Kwa hiyo mie nikifanya overtime zangu na kupokea hela yote nikaamua kumpelekea mtumishi leo ili asiende shambani akahubiri ni mjinga?
 

ni kweli sio marufuku kutembelea hammer kwa mchungaji.. lakini mimi ningekuuliza swali moja.. we umesema umesali hapo ubungo kwahiyo obvious inaonesha unamwamini yesu.. na unaamini anauwezo wa yote swali je kipindi kile yesu amekuja kulikuwa na vitu vya fahari yesu alikuwa anatoka mji hadi mji kwenda kuhubiri neno.. hivi kwani yesu asingeshindwa kuwa na farasi wa ukweli (au a carriage).. ili kumrahisishia usafiri na pia badala ya kulala sehemu nyingine angekuwa anafikia motels au gesti house...

same thing kwake paul, alivyokuwa anahangaika kwenda drom place to plave kwani alishindwa kuwa na vitu vyotehivi?


kwahiyo haojamaa wanahubiri utajirii.. wanahubiri injili???? nadhani hapa ndo tatizo linapoanza.. watu wanenda kwenye makanisa kuhubiriwa utajiri sio kuhubiriwa injili.. au sio???
 
Labda kwa makanisa ya Katoriki na Lutheran lakini makanisa ya kipentekoste wako wazi kwa masuala ya pesa na wala wachungaji hawahusiki kabisa katika masuala ya pesa.

ni kweli, wachungaji hawahusiki kuna watendaji wa kanisa ambao wanahusika na wanapanga matumizi ya pesa kwa nia ya kuendeleaza kanisa, sioni sababu ya mtumishi wa Mungu kutokuwa na gari la maana,
 
SIO SIRI MUNGU ANAHUZUNIKA SANA.KWELI VIONGOZ WA DINI WANATANUA KWA MABILION TOKA KWA MICHANGO JAMAN THAT IS Y MIM NATUMIA ASILIMIA 95% YA FEDHA YANGU KUWAPA MASIKIN KULIKO PELEKA KANISAN NAKUPIGIWA MAKOFI. INAMUUMA SANA SANA SANA MUNGU WATU HAWANA KITU ILA WANAKAMULIWA MPAKA WANASEMA HV KWEL MUNGU NDIO ALIVYO AU? WANATUMIA KITABU CHA MALAK KUKAMUA WATU HATA HVYO KUMTOLEA MUNGU NI MOYO WA KWEL TOKA KWA WATU WA MUNGU, WATOAJI NIWATOAJI WALA HAWANA AJA YA MANENO MENG WANAMTOLEA MUNGU VYOTE WANAVYO KWA MOYO WOTE. Mungu fanya mabadiliko ktk kanisa Tanzania.
 
 
Ni kweli ndugu yangu wako wanaofanya hivyo lakini je kama unaamini Mungu basi ifunike kwa damu ya Yesu na ombea hela yako imfikie mlengwa na kzia Mungu amkemee yule mwovu asiile hiyo sadaka yako, ukiona mtumishi wako ni mwizi basi ondoka, mwombe Mungu akupatie mahali sahihi pa kuabudu.
Mfano kwangu sasa hivi kuna list kabisa ya yatima, wajane na wasiojiweza inawekwa kwenye notisi board na mtu ukivutwa waweza toa, mchukua au saidia chochote, lakini moyo wa kutoa sio lazima iwe kanisani hata mitaani tunaishi nao na tunapaswa kuwasaidia pia bila ubaguzi, kwa hiyo Mungu anaona bila kujali umetolea wapi.
 

Yesu angekuwa wakwanza kutanua kama tajiri kuwa mfano wa hao wanaji ita wachungaji, kila unapo soma juu ya Yesu utaona anaimiza watu kusaidiana nakama una kanzu moja umpe namwenzako Je hawa viongoz wanafundisha nin kama sio umimi nakuwa acha watu masikin pasipo dira. Kanisa lazima lisimame nakuwa kimbilio la watu wasio kuwa na kitu lakini leo masikin anazid kuwa masikini wapi tunaenda, tunajanga la watoto wa mitaani, wajane na mayatima viongoz hawa wanakula tu tena kwa amani Je huo ni uungwana? Tunajenga kanisa au watoto wa mafisadi ndan ya kanisa. Dhati is y wanakuwa wa kwanza kupinga ukatwaji wa kodi ktk makanisa. I'm sorry kama kiongoz kanisa ningelinjoosha kwavile wameshindwa kujiongoza so sasa sis serikal tunaingilia kati. Kwel jaman tuwe na huruma hata Yesu akasema yakaisari mpe kaisari, na Yake Mungu mpe MUNGU JE INA MAANA KUNA VAT NA KODI MBILI YA DUNIANI NA MBINGUNI? Bila shaka hakuna Yesu akutembeza bakuli lakuomba omba na anajidhihirisha ktk arus ya Kana na kule bustanin ambapo alifanya mikate kumultply wakala maelfu. KANISA NILAZIMA LI CHANGE NAKAMA HAWAWEZI MUDA UNAKUJA WATABADILISHWA KWA NGUVU KUTOKA JUU. Mungu ibariki Tanzania..
 

Ukiamua kuchukua overtime yako yote ukampelekea mtumishi wakati bado una mahitaji yako mengine utakuwa mpumbavu sana. Siku hizi kila kitu ni kazi, asilimia kubwa ya wachungaji na maaskofu wamekuwa tu hivyo maana ni ajira ambayo hulipi kodi TRA. Wamebaki wachache sana ambao wanamtumikia Mungu kikweli bila kuangalia maslahi yao binafsi kwanza. Unataka kuniambia magari yote duniani yameisha mpaka ununue gari ya 250ml? na kwamba waumini wote wa huyo askofu wanajimudu kimaisha? Mnanyonywa bado mnanyonyeka tu.
 
Hivi fungu la 10% na sadaka kanisani nani ane kula haswa? Zinaenda wapi kwa Mungu au wapi? Maana utasikia toa ndugu toa ulicho nacho ukikificha Mungu anaona wapi sasa zinako elekea nani anakula au kufaidi pesa za kanisa?
 
wajinga ndio waliwao......wanaojiita wachungaji wote wezi na matapeli tu.

ikiitumia akili visivyo(kijinga) itakuletea madhara na ukiitumia vyema itakupatia faida,

kunena pasipo mipaka kutakufanyia nyakati mbaya kwako, angalia useme nini na lipi ukae kimya. Take care
 
Tatizo tulio wengi tunamtazamo mfupi, na husuda zimejaa mawazoni mwetu hatuuoni ukweli, ndio maana tunalalamika kwa mambo dhahiri. Mkuki mtamu kwa ......ila kwa binadamu mchungu. Mtu hutaka vizuri daima na hutegemea kuvipata pale alipo, wewe pia. Kama vile; Baba Askofu huyo anapokwenda kuweka wese la sh. 300k kwa siku; wengi hufaidika kwa mshahara kutokana na wese hilo kutoka lilikochimbwa, kusafirishwa , kusafisha hadi kuuzwa. Wengi wamekula, wamesomesha watoto, wanastarehe kwa hilo na mengi mengineyo. kwa huyu Baba ni ni ile sifa tu kwa wasioona mbali. Sisi tunaoona mbali hili ni jambo jema na linamanufaa wa wengi ingawa huwaoni. Nadhani wewe umenielewa. Hakuna baya hapo ni mtazamo wako wa uchoyo na umimi ndio unahukumu vibaya. Mwache mtumishi awatumikie watu wote ulimwenguni vema banaaaaa.
 

A righteous person's(including a preacher) Compensation is heaven and eternal life not money worthy..
 
overtime ni zaidi ya mshahara wangu, na ukisema hadi umalize mahitaji yako yote, kweli kuna kitu utapeleka kwa mungu?
Mie kadri ninavyotoa ninapokea maradufu, na pia sina hofu kwani najua mbingu na nchi vyote ni mali ya bwana, na alisema hatanipungukia wala hataniacha, hata nikianguka nitasimama tena ivo sina hofu ya kumtolea mungu mradi nijue ni matumizi sahihi, lakini nikisikia tu watunza fedha au kanisa linalalamika mtumishi anatumia hela ya kanisa vibaya basi nitaacha. Pia tunaenda kiroho kwa hiyo utakuta unachotoa ni kwa kazi maalumu ya mungu sio unatoa tu kama njugu nakubaki unalalamika kama tunavyotozwa kodi serikalini. Tuna amani kabisa.
 

kwahiyo unataka kusema kwamba umaskini ni result ya dhambi na utajiri ni result ya kuwa mcha mungu... ???? unanikumbusha ile hadithi ya yule mtoza ushuru na mfarisayo walioenda kusali Luke 18: 9-12..
 
They need to controbute taxes to the nation basket.
Hata msemeji huo ni wizi wa mchana na kuwapoteza wadanganyika ambao wengi wanafrustration za ufukara, hali ngumu ya maisha, magonjwa ya ajabu ajabu, kunyanyaswa na serikali zao, etc, etc. Kuwepo na utaratibu wa taxation kwa religion organisations ikilenga exemption ya kodi kwa vile vitu tu, vinavyoendana na ibada, mfano ujenzi wa kanisa, vyombo vya kuendeshea ibada, etc, na kuwepo na accounting system kanisani ili kuhakikisha kuwa kanisa nalo linalipa kodi stahiki kama linamapato na linafanya biashara (hoteli, benki, maduka, kupangisha nyumba, etc). Vyombo vya dini nazo zilipe kodi kwa vile vitu ambavyo zinaingiza fedha na zinaleta ushindani sokoni ili kuwa na level playing field.
 
Hivi fungu la 10% na sadaka kanisani nani ane kula haswa? Zinaenda wapi kwa Mungu au wapi? Maana utasikia toa ndugu toa ulicho nacho ukikificha Mungu anaona wapi sasa zinako elekea nani anakula au kufaidi pesa za kanisa?

KAMA WEWE NI MKRISTO BASI KASOME KITABU CHA MALAKI NA JEREMIAH utaelewa zaidi.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…