Askofu Bagonza: Anayetugawa hawezi kutuunganisha

Baba askofu nakupongeza. Itikadi ni imani. Leo watu wanalazimishwa kuwa na itikadi moja kwa kuambiwa wasipofanya hivyo huduma kwao basi. Wanaweza wakakuaminisha kwa kuvaa sare kitambulisho cha itikadi yako, mioyo yao hutaibadiri. Serikali utimize majukumu yake kwa wananchi bila kujali itikadi zao.
 
Baba Askofu Bagonza MUNGU aendelee kukutunza na kukuongezea Imani.
Naumia Sana binadamu kuukwepa ukweli.
Hebu pitieni hoja za Pascal Mayalla kwenye mada na Ni mwanachama wa ccm ambaye anatamka ahadi ya nitasema kweli daima fitina kwangu Ni mwiko!
 
Kwa Mara ya kwanza natofautiana na Askofu Bangonza.

Tofauti za dini zimeligawa taifa.

Pamoja na Serikali kujipambanua haina dini na haipendelei wala kubagua dini, hata hivyo Serikali inapendelea dini.

Hii inathibitishwa pia na tafiti kutoka kwa shirika la tafiti linaloheshika duniani.

Many Countries Favor Specific Religions

Tofauti ya rangi ya ngozi ya mwili imeligawa Taifa. Tokea uhuru, hatujasikia watz wenye asili ya Asia na arabuni wakipata teuzi ktk nafasi za maamuzi.

Mengine tuko sawa.
 
Hako kajichumba ka'pale Posta House pia kalimshinda kulipa, hali ikawa ngumu sana kiasi ofisini penyewe pakawa hapakaliki ni ukata na vumbi tu ndio vilitawala

Baada ya kushindwa kulipa uongozi wa Jengo la Posta ukakabidhi deni kwa kampuni ya udalali inayoitwa MSOLOPA ambapo baada ya miaka miwili kupita ilibidi wavunje ofisi na kuchukua vilivyomo na kuvipiga mnada

Kapoteza heshima, pia kapoteza uelekeo anasubiri kudra za Magufuli apewe uteuzi

Kayumba vibaya sana
 
Mkuu AGITATOR , usiwajali vibaraka hawa, mwisho wao ni October 28, watalia sana!.
P
Yaani na wewe unaunga mkono mchana kweupe propoganda mfu za 'mabeberu'? Juzi kati watu walitembeza klipu yako ukimuuliza jiwe swali lililokwenda shule katika press conference ya Ikulu mwanzoni mwa utawala wake - kwa hakika kila mmoja aliona hapa tuna wanahabari. Alishindwa kujibu na akaishia kutafisiri jina lako katika lugha ya Kisukuma. Ama kweli njaa imekuingia kichwani. Huu ni mfano hai wa hoja ya Baba Askofu. Mtu mweledi na mpenzi wa kuitendea haki profession yako, baada ya miaka mitano you have been reduced to mediocrity!!!
 
Mkuu AGITATOR , usiwajali vibaraka hawa, mwisho wao ni October 28, watalia sana!.
P
Nijuavyo mimi na wewe pia ni muhanga wa hilo ndio mana ilifikia mahali MSOLOPA wakakuvunjia ofisi kutokana na deni sugu la kodi baada ya mambo kuyumba kuanzia mwaka 2016

Ila unajikaza kisabuni kumlamba miguu Farao ili upate uteuzi angalau ujuweke sawa umeshaa sana bro!
 
Hiyo No. 3 ndiyo tunayoishuhudia, Mungu atunusuru
 

Kipindi nipo karagwe na soma kule huyu askofu bagonza yeye kila mtawala amkubali .sijui marekani wali mfanya nini ?
 
ANAYETUGAWA HAWEZI KUTUUNGANISHA

Tofauti za dini zilishindwa kutugawa. Serikali haina dini na hakuna anayelazimishwa kuwa na dini.

Tofauti za makabila zilishindwa kuligawa Taifa. Makabila madogo yana fursa sawa kama makabila makubwa. Faida ya makabila ni kutambika na kufanya fujo katika misiba ya watani.

Tofauti ya rangi ya ngozi ya mwili haikuligawa Taifa. Baada wa kupata uhuru, baadhi ya waliokuwa wanaitwa wakoloni waliteuliwa kuwa mawaziri. Binadamu wote ni ndugu zangu na Afrika ni moja.

Tofauti za vipato hazikuligawa Taifa. Tajiri na maskini wanaweza kunyea ndoo moja huko mahabusu. Utajiri ni wa mtu lakini umaskini ni wa Taifa. Aliyewapa hawa ndiye kawanyima wale.

Tofauti za kiitikadi zinaligawa na kulisambaratisha taifa letu. Kwa nini?

1. Tofauti za kiitikadi zaweza kukutia hatiani au kukuweka huru.

2. Tofauti za kiitikadi zaweza kukupa au kukunyima maji ya bomba, barabara, HOSPITALI na
Shule.

3. Tofauti za kiitikadi zaweza kumpa uongozi kichaa na kumnyima Profesa kazi hiyo. Chama kinakuwa bora kuliko mtu. Hatuko salama.

4. Chama kinakuwa na nguvu kuliko Muumba. Mmoja amependekeza akishinda atabadili jina la nchi liwe la chama chake! Mitume hawasikilizwi lakini makada wanashangiliwa. Ukame ukija tusitafutane.

Viongozi wa dini ombeeni na kugawa baraka kwa rangi zote. Wanyambo walisema "Lisha mbwa wote washibe kwa usawa na bila upendeleo maana hujui ni yupi atakayewinda vizuri na kupata mawindo". Na watani wangu wa Tarime husema, "Asiyetembelea kwa mtemi huwa ananungunika eti mtemi ni bahili".
 
Mkuu AGITATOR , usiwajali vibaraka hawa, mwisho wao ni October 28, watalia sana!.
P
Mwalimu Nyerere alishasema "Tunawapinga MAKABURU kwasababu za UBAGUZI wao". Kiongozi hawezi sema "msinichanganyie, mkaniletea upinzani, mara sitoleta maji, n.k.". Natumai hata wewe kwenye familia yako kuna jinsi KE weusi, wakidhulumiwa haki zao, mafao hawatasikilizwa pia.

Sent from my SM-G900F using JamiiForums mobile app
 
Ana tabia ya ku-like kila post inayosukuma zaidi dawa ya sindano iliyomwingia vizuri takon.i mwake na akawa hana majibu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…