Pre GE2025 Askofu Bagonza ataka walimu wasio na ajira (NETO) wasikilizwe na siyo kukamatwa na kutishwa

Pre GE2025 Askofu Bagonza ataka walimu wasio na ajira (NETO) wasikilizwe na siyo kukamatwa na kutishwa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

the guardian 17

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2024
Posts
395
Reaction score
570
Askofu wa Kanisa la KKKT Dayosisi ya Karagwe, Askofu Benson Bagonza achukizwa na kamata kamatwa inayofanywa na Jeshi la Polisi kwa Viongozi wa Walimu wasio na ajira ambao wamejitokeza kuikumbusha Serikali juu ya hatma yao ya haki ya kupata ajira ambayo wameisubiri kwa muda mrefu tangu walipo maliza masomo yao, wengine walihitimu tangu mwaka 2015 mpaka hivi sasa hawajapata ajira.

Soma: Mwenyekiti wa Walimu Wasio Na Ajira (NETO) Joseph Paulo anadaiwa kukamatwa na polisi mkoani Geita

"Kwahiyo hapa tunazungumzia kundi ambalo, tuna walimu wengi wasioajiriwa kuliko walioajriwa na hii siyo sawa. Kwahiyo mazungumzo, maridhiano yanatakiwa na kundi hilo kuliko kuwakamatakamata, kuwatishatisha, kuwalza ndani. Sasa mtu ana njaa unamlaza ndani hana kazi, ukimlaza ndani ndiyo kazi ameipata?" - Askofu Bagonza

Kupata taarifa na matukio ya kimkoa kuhusu Uchaguzi Serikali za Mitaa ingia hapa: LGE2024 - Special Thread: Orodha ya Mijadala ya Mikoa yote Tanzania Bara inayoshiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
 
Hapa kikubwa ni kuacha kusoma TU na kuendelea kupiga mitungi TU!!!
 
Back
Top Bottom