Askofu wa Kanisa la KKKT Dayosisi ya Karagwe, Askofu Benson Bagonza achukizwa na kamata kamatwa inayofanywa na Jeshi la Polisi kwa Viongozi wa Walimu wasio na ajira ambao wamejitokeza kuikumbusha Serikali juu ya hatma yao ya haki ya kupata ajira ambayo wameisubiri kwa muda mrefu tangu walipo maliza masomo yao, wengine walihitimu tangu mwaka 2015 mpaka hivi sasa hawajapata ajira.
"Kwahiyo hapa tunazungumzia kundi ambalo, tuna walimu wengi wasioajiriwa kuliko walioajriwa na hii siyo sawa. Kwahiyo mazungumzo, maridhiano yanatakiwa na kundi hilo kuliko kuwakamatakamata, kuwatishatisha, kuwalza ndani. Sasa mtu ana njaa unamlaza ndani hana kazi, ukimlaza ndani ndiyo kazi ameipata?" - Askofu Bagonza