benzemah
JF-Expert Member
- Nov 19, 2014
- 1,533
- 3,187
Watunzi wa vitabu na waandishi wa habari wametaki wa kuandika uhalisia kwa kufanya utafiti.na uchunguzi wa kuto sha ili kupata ukweli wa mambo badala ya kuandika kwa mihemko, jazba na visasi hali itakayosababisha. walaji wasipate kile kilichokusudiwa.
"Watanzania hawakuchagua malaika, wanaweza kuandika historia ya matendo yao na kuongeza kuwa kunahitajika zijengwe taasisi imara zitakazowasimamia na kuwadhibiti viongozi ili wasitumie madaraka yao vibaya," alisema Askofu Bagonza
Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Karagwe, Dk Benson Bagonza alisema hayo jana baada ya kuzindua Kitabu cha 'I am the State' (Mimi ndiye dola) kilichoandikwa na mwanahabari Ansbert Ngurumo kwa kushirikiana na wanahabari wenzake; Absalom Kibanda, Nevile Meena na Jesse Kwayu.
Dk Bagonza aliyekuwa mgeni rasmi, alisema hata wasomaji wa kitabu hicho na kupingana na maudhui yake waje na hoja madhubuti zinazothibitika kinadharia na kivitendo ili kutoyumbisha ukweli uliofanyiwa kazi na watunzi wa kitabu hicho.
Aliwataka Watanzania kuanza kuandika vitabu vya maisha ya viongozi hata kama viongozi hao wameshaanza kuandika historia ya maisha yao wakati wakiwa madarakani ili mradi utafiti wa kutosha ufanyike ili viongozi hao wasionewe.