Askofu Bagonza: CCM huwa hawachagui Mwenyekiti, wanateua Mgombea Urais wanamteka kuwa Mwenyekiti wao

Mtoa Taarifa

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2024
Posts
213
Reaction score
671

Vyama vyote vya siasa hapa nchini ni vyama vya viongozi, siyo vyama vya wanachama. Vyama vyetu vya siasa hapa nchini vina tatizo moja kubwa, ni vyama vya viongozi sio vyama vya wanachama. Matashi ya wanachama hayaheshimiwi na viongozi, kwahiyo nani anagombea nani hagombei kwangu siyo tatizo, tatizo nililonalo ni kwamba michakato ya kidemokrasia ndani ya vyama vya siasa hapa nchini bado ina kasoro kubwa kwasababu inaruhusu viongozi kumiliki vyama badala ya wanachama kumiliki vyama.

Jambo la pili kwa kulinganisha CHADEMA na CCM, hata ndani ya CCM huwa hawachagui Mwenyekiti wanasubiri wanapoteua mtu kugombea na kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kisha wanamteka anakuwa mwenyekiti wao, kwahiyo sidhani kama CCM ni ‘model’ nzuri ya kuchagua viongozi wa chama kwasababu hata sehemu kubwa ya wajumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho siyo wa kuchaguliwa bali ni wale wanaoingia kwa nafasi zao, kwahiyo wanatumia itifaki zaidi kuliko demokrasia ndani ya CCM"- Ask. Bagonza.

Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Karagwe Dkt. Benson Bagonza akizungumza na kituo cha habari cha SAUT Digital, kutokana na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tundu Lissu kutangaza kuwania nafasi ya uenyekiti wa chama hicho ngazi ya taifa, wakati wa mkutano na wanahabari uliofanyika Alhamisi tarehe 12 Desemba 2024.
 
Well said.
CHADEMA imeonyesha njia watu wamepagawa.
 
MshAuli mbowe naye afanye hivi over
 
Demokrasia ni kuwa kila.mmoja agombee. Sifa iwe moja tu, kuwa mwanachama hata hajui kusoma na kuandika agombee as long as ni mwanachama🤣🤣🤣😃😂😁😄😊
BASI
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…