Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Karagwe, Dkt. Benson Bagonza, ameonyesha wasiwasi wake juu ya hali ya demokrasia ndani ya vyama vya siasa nchini, akisisitiza kuwa vyama vingi vimejikita katika kuongozwa na viongozi badala ya kuheshimu matakwa ya wanachama.
"Vyama vyote vya siasa hapa nchini ni vyama vya viongozi, siyo vyama vya wanachama. Matashi ya wanachama hayaheshimiwi na viongozi, jambo ambalo linaathiri michakato ya kidemokrasia," alisema Askofu Bagonza akizungumza na kituo cha habari cha SAUT Digital.
Kwa mujibu wa Bagonza, tatizo kubwa ni kwamba michakato ya kidemokrasia ndani ya vyama vya siasa bado ina kasoro, kwani inaruhusu viongozi kumiliki vyama badala ya wanachama kuwa wamiliki halali.
Akiizungumzia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Askofu Bagonza alisema: "Hata ndani ya CCM, mwenyekiti wa chama siyo chaguo la wanachama bali huchaguliwa baada ya kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hili linaonyesha kuwa CCM si mfano mzuri wa kidemokrasia ndani ya vyama."
Aidha, Bagonza aliongeza kuwa sehemu kubwa ya wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM huingia kutokana na nafasi zao za uongozi, hivyo kutumia itifaki zaidi kuliko demokrasia.
Kauli hiyo ya Bagonza ilitolewa wakati wa mahojiano kufuatia tangazo la Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, la kugombea nafasi ya uenyekiti wa chama hicho ngazi ya taifa, alilolitoa katika mkutano na wanahabari uliofanyika Alhamisi, tarehe 12 Desemba 2024.