Askofu Bagonza: Haki na Uhuru vimeumana

Askofu Bagonza: Haki na Uhuru vimeumana

BAK

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2007
Posts
124,790
Reaction score
288,165
HAKI na UHURU VIMEUMANA!

Maneno "haki" na "uhuru" yameanza kusikika kwa kasi toka midomoni mwa watawala na Viongozi wetu. NAWAPONGEZA.

Hakuna aliyepiga marufuku matumizi ya maneno haya lakini si kila marufuku inatolewa hadharani. Taifa lilishtuka pale tulipoona haya:

1. Watawala waliposisitiza zaidi "uhuru wenye mipaka" badala ya uhuru wenyewe.

2. Walisisitiza "amani" kuliko haki.

3. Wakasisitiza "wajibu" kuliko haki.

4. Kazi ya bunge ikawa ya "kuishauri" serikali na SI "kuisimamia".

Matokeo yake tukapata haya:

i. Utulivu usio na amani

ii. Utumwa mstaarabu

III. Nidhamu ya woga

iv. Matumizi ya nguvu kuliko akili

v. Matumizi ya Vikosi Kazi badala ya mfumo-kazi.

vi. Wakuu wa mikoa na Wilaya wakawapa wabunge masaa 24 warudi bungeni vingine watatiwa pingu

vii. Spika akawa na nguvu kuliko bunge, Rais akawa na nguvu kuliko nchi na wananchi wakawa chini ya vyote.

Sasa hivi wakuu wa mikoa wanatamka neno HAKI. Spika anazungumzia "watu wajimwage wasikie wana nafasi". IGP anawaambia maaskari watende haki na kuelimisha badala ya "notification".

Naamini hata Msajili wa vyama ataanza kutafuta neno HAKI lilienda wapi. Vyama vya siasa vitaachana na kunyonya titi la vyombo vya dola. Wabunge wataiacha serikali ijitetee ili wao waisimamie.

Rais wetu asiingizwe wala yeye mwenyewe kuingia jikoni kwa vitu vidogo (micromanagement). Tulifika mbali, hata wanaume kuchelewa kurudi nyumbani anaambiwa Rais!!

"Kwa mtu mmoja dhambi iliingia na hatimaye MAUTI... na kwa mtu mmoja wokovu ulirejea" (Warumi 5: 12-21).​


1622069048609.jpeg
 
CCM huwa wanabadilika kulingana na tabia ya mwenyekiti wao, akiwa katili nao watakuwa katili zaidi yake ili kumuonesha wanajua zaidi kufanya anachopenda, na mtawala akiwa mpole jamaa wanabadilika hapo hapo.

Tungepata Katiba Mpya ingetuondolea huu utumwa wa fikra ulioota mizizi ndani ya CCM kwani kila mmoja angetimiza majukumu yake kwa kulindwa/ongozwa na sheria, na sio kwa mapenzi ya mtu.
 
Namba 2 ilikuwa inanikera Sana, unawezaje kusisitiza amani kwa watu unaowadhulumu haki yao?
 
CCM imezeeka hivyo inajiendea ili mradi bora liende. Sasa tuikatae au kuilazimisha ife

 
Hakika giza limetoweka Nuru inaangaza Taifa sasa linapumua tulikua kama tuko utumwani au kama shuleni kila jambo tunasubili amli toka kwa mwalimu au kwa kilanja
 
Back
Top Bottom