Nilichogundua WATZ wana uelewa mdogo (finyu) sana kwenye masuala ya kikodi na sheria zake kwa ujumla. Wengi kabla ya kupost huwa hawafanyi utafiti ili kujipa nafasi kubwa zaidi ya kuelewa nini hasa kinapaswa kuandikwa.
Kodi ya majengo ilibadilishwa kutoka serikali za mitaa kuja Serikali kuu (TRA) mwaka 2016/2017. Property tax inatoswa tu kwenye NYUMBA za kudumu na zilizopo kwenye ( MAJIJI, MANISPAA, HALMASHAURI ZA MIJI, NA MIJI)
Kodi hii haitozwi nyumba za zilizopo VIJIJINI hata kama umejenga ghorofa huko. Mfano ile nyumba ya MENGI kule kijijini kwao hailipiwi kodi ya jengo.
VIWANGO VYA KODI.
1. 12,000 kwa nyumba za kawaida kwa mwaka
2. 60,000 kwa kila sakafu moja ya nyumba za ghorofa.
Misamaha ya kodi ya jengo.
Hapa kuna makundi kadhaa hupewa msamaha wa kodi hii.
1. Wazee wenye umri wa miaka 60 kwenda juu. Hawa hawalipi kodi hii na anapaswa kuomba msamaha huo kila mwaka. Lakini ikiwa ana nyumba ambayo amepangisha kibishara atalazimika kulipia kodi ya jengo.
2. Mashirika ya Dini, UN, SADC, JUMUIYA ya Madola na mashirika yanayoendana na hayo hayalipiwi kodi hiyo pia.
3. Shule, hospitali, majengo ya umma (serikali) hayalipiwi kodi ya jengo. Hapa ieleweke kuwa yapo majengo ya mashirika ya umma ambayo hulipiwa kodi ambayo yako kibiashara. Mfano nyumba za NSSF, NHC, POSTA, BOT nk hawa wanalipia kodi maana wao hutumia hizo nyumba kibiashara kwa kupangisha watu wao.
KUHUSU MALIPO KWA NJIA YA LUKU.
Ieleweke wazi kuwa moja ya sifa kuu ya kodi ni utumiaji wa gharama ndogo katika kukusanya kiasi kikubwa cha kodi. Zamani tulikuwa tunatumia gharama kubwa kukusanya kodi hii lkn pia mlipaji mwenyewe hutumia gharama kiasi kuja kufauata bill yake ili aweze lipia. Mfano mtu atoke MGENI NANI (MBAGALA) aje ofisi za TRA TEMEKE ili apeww bill yake ya jengo ya Tsh 10,000 ndio akalipie, hali hii ilichangia ufanisi mdogo na kukusanya mapato haya chini ya 50% karibia kila mwaka.
Hivyo basi utaratibu huu umewekwa mahsusi ili kuondoa mikwamo hiyo na kuondoa ukwepaji kodi kwa kiwango kikubwa. Kodi hii sasa itakatwa mara moja tu kwa mwezi yaani mara ya kwanza utapoweka umeme katika kila mwezi basi utakatwa 1000 kwa nyumba ya kawaida na 5000 kwa ghorofa kwa kila sakafu moja.
Ikumbukwe kuwa kodi hii hukatwa kila nyumba moja na sio kila LUKU ya nyumba husika. Hivyo kama nyumba ina mita za LUKU zaidi ya moja unapaswa kufika TRA na property reference no yako pamoja na mita namba zako ili kuweza kuziondoa ibakie moja ambayo itakatwa hiyo kodi.
Kwa wale ambao wana nyumba za kudumu na zipo maeneo ambayo hulipiwa kodi za majengo na hawana umeme basi watalazimika kutumia utaratibu uleule wa zamani mapaka pale watakapovutia umeme.
KWA UCHACHE NAWEZA KUSEMA WENGI MTAANZA KUELEWA HII KODI. NA NAIMANI TUTAKUWA PAMOJA KATIKA KUIJENGA NCHI YETU HII ILI TUENDELEE KUBORESHA MIUNDOMBINU YETU, HUDUMA ZA JAMII NK.
AHSANTENI.