3KUTOKA KIKOMBE CHA BABU hadi MAFUTA YA UPAKO
NI Jumapili 6/7/2025, Wakristo tumeenda makanisani, Mahemani na mahekaluni. Uhuru wa kuabudu tunao mpaka unafurika! Hata kuabudu wakati unalia, unarukaruka, unapigwa mabomu, umekanyaga mafuta, unachapwa viboko, yote sawa.
1. Mungu huwainua watumishi kwa wakati na kwa kusudi maalum. Yeye habadiliki lakini sisi tunabadilika. Kusudi lake laweza kubadilika kwa wakati unaobadilika.
2. Tunaonywa: Tusiwekeze imani yetu ya kudumu kwa kusudi la muda. Watumishi hupita, Mungu akabaki.
3. Alikuwapo Ambilikile Mwaisapile (Mzee wa Kikombe cha Loliondo). Watu waliacha makanisa; wakaacha miiko yao; wakaacha itifaki zao - Wakaenda Loliondo kukinywa kikombe.
4. Mataifa mbalimbali yakatiririka kwenda Loliondo. Marais, maaskofu, mitume wa kweli na feki; madaktari, mawaziri na dini zote, WAKABUGIA KIKOMBE. Waliojulikana kwa kuombea wagonjwa, wakazomewa na wateja wao walioenda kunywa kikombe. Hawakujua kuwa kikombe ni tunda la msimu.
5. Kimataifa tumewahi kuwa na Benny Hinn, Jim Swaggat na Bill Graham. Waliinuliwa. Kusudi la Mungu lilipobadilika walishuka. Wengine waliinuliwa baadaye wakajiinua. Wakashushwa kama gunia la Lumbesa lisilo na mpokeaji.
6. Walioinuliwa na kushushwa pamoja; na waliojiinua wakashushwa, walishuka na wafuasi waliowaamini wao kuliko walivyomwamini Mungu. Hakuna umilele katika mtu, kitu wala hali. Umilele ni kwake aliye wa milele - MUNGU MWENYEZI.
7. Tulikiamini kikombe. Kilipita, tukabaki. Majuto yapo lakini hayatuzuii kuamini mafuta, chumvi, nywele, maji, udongo, suruali, keki na juice. USIDIRIKI kumzuia aliyemwamini mleta kikombe wala mafuta. Unapoteza muda kama ninavyoupoteza. Muda ni hakimu asiyehongwa.
8. Imani ni kitu ingine - achana nayo. Tuliamini mapangoni, ikapita. Tukajenga mahekalu, bado ugumu wa mioyo ukabaki. Wasomi wakatangaza kifo cha Mungu. Wakafa na Mungu akabaki. Maadui wakachoma makanisa, wafalme wakaua manabii, wakristo wakazushiwa wanakula nyama ya mtu. Kanisa likabaki, wazushi wakazikwa na kanisa. Bado hatujifunzi!?
9. Kanisa la kweli ni nini? Linalosali kwenye mahekalu ya dhahabu? Chini ya mti? Hemani? Ukumbi wa hotel? Chumba cha Darasa? Kwenye bar? Linaloogopa Polisi? Lisiloogopa polisi? Lenye watu wengi au wachache? Nijuacho: Hakuna anayelijua kanisa halafu akalishambulia.
10. Yesu akasema, “nitalijenga kanisa langu, wala nguvu za kuzimu hazitaliweza kamwe” (Mathayo 16:18). Tangu siku hiyo, siyo simba, dubu, kitanzi, upanga, kifungo, risasi, moto, marufuku, bomu, umaskini, utajiri, mamlaka, wala uchawi unaweza kulimaliza kanisa. Huduma (Ministry) zaweza kukoma lakini kanisa halisi au la nadharia haliwezi kukoma. Liwe jengoni, hemani, pangoni, au angani, litabaki.
11. Kanisa ni la nyakati zote (all seasons). Ukilichukia umejichukia. Ukilipenda umejipenda. Liliwakumbatia wakoloni; walipoondoka likawabariki wakombozi. Itikadi zote rafiki na hasimu hufanya kazi na kanisa. Linapenda kufundisha si kufundishwa na mwanadamu. Mwalimu wake ni Kristu. Linaweza kuteseka kwa kiburi chake, lakini tutambue kuwa ni Mwili kamili wa Kristu (La kibinadamu na Kimungu wakati ule ule).
12. Analijua vizuri muasisi wake Yesu Kristo. Watumishi twajua sehemu ndogo. Tutabakia wanafunzi bila kuhitimu. Nguvu yake si idadi wala majengo. Nguvu ya kanisa ni kusema ukweli uwekao huru. Uhuru uliojengwa katika haki iletayo amani. Udhaifu wake ndiyo nguvu yake. Jihoji unapomtesa anayekuombea.
Ni kwa hisani ya Mchg ANICET MUTATINA MAGANYA, aliyeadhimisha jubilee ya miaka 20 ya daraja la huduma ya Uchungaji leo 6/7/2025.
UPuuzi mtupu. Samia hana nafasi ya kulipandisha Kanisa la Kristo. Mwamposa anapandishwa na Samia kwenye biashara yao najisi ya mafuta, udongo na maji.Kapata kijiba cha roho kuona Mwamposa akipanda
Wajinga wacha wajae Kwa Mwamposa watakavyo lakini siku inakuja watalia na kusaga Meno. Kanisa la Karne hii halimtaji Yesu?Kapata kijiba cha roho kuona Mwamposa akipanda
Bangonza hana haja ya kubembeleza waumini maana wao wapo tu, KKKT sio kama makanisa ya upako yanayo tapeli watu kwa mafuta na matakataka mengineBagonza yuko katika promotion ya biashara yake ili waumini (wateja) wasimkimbie.
Amezungumza mambo mazito sana.... Uhuru uletao HAKI, Amani na maendeleo!Bagonza yuko katika promotion ya biashara yake ili waumini (wateja) wasimkimbie.
Ebu mwambie huyu chawa mpauko!Bangonza hana haja ya kubembeleza waumini maana wao wapo tu, KKKT sio kama makanisa ya upako yanayo tapeli watu kwa mafuta na matakataka mengine
Kwani kamtaja mtu?Kapata kijiba cha roho kuona Mwamposa akipanda
Umesoma vzr kabla ya kuchangia?.Kapata kijiba cha roho kuona Mwamposa akipanda
Inasaidia nini wakati waumini wake kwake maskiniFalsafa tupu
Tupo DRC kinshasaKUTOKA KIKOMBE CHA BABU hadi MAFUTA YA UPAKO