GE2025 Askofu Bagonza: MKEKA WA CCM, Mashaka ni Mengi Kuliko Matumaini

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,186
Reaction score
4,940
Anaandika Askofu Kalikawe Lwakalinda Bagonza kupitia ukurasa wake wa Facebook.
====

MKEKA WA CCM: Mashaka ni Mengi Kuliko Matumaini.

CCM ni kama Marekani. Uchaguzi wake unawala macho hata wasiohusika. Leo mkeka umeshangaza watu. Mimi nimejikaza na kufanikiwa kutafakari haya:

1. Waliokatwa nawapa hongera. YAWEZEKANA Mmeepushwa na jambo baya mbele yenu. Kama lipo, mmepona. Kama halipo, wanalaumiwa waliowakata. Furahini katika Bwana tena kwa furaha.

2. Waliopenya msishangilie. Waliokatwa leo, waliwahi kushangilia. Mnafikiri mna jipya?! Kuna wajunbe wanawasubiri. Kuna fitna zimeandaliwa. Hata wagumba watasingiziwa wametoa mimba! Siasa zetu ni chafu lakini zinapendwa. Kama siyo mchafu unatafuta nini huko?

3. Kwa nini kanuni ya watatu haikuachwa itumike angalau uchaguzi mmoja tuione mazuri na mabaya yake? Ilileta kelele. Hata hii haina utulivu. Kuna kuyumba katika maamuzi. Kambarage alionya, “CCM ikiyumba, Taifa litayumba”. Tumeishayumba ndo maana kila mmoja kafunga mkanda na kukaza macho.

4. Haki na Usawa vimeshindikana kote. Ma DC, Ma DED na Ma RC walijiuzuru ili kugombea ubunge. Lakini wabunge wa Afrika Mashariki hawakujiuzuru! Au mnadhani watashindwa? Kanuni zetu zina macho na pua.

5. Hivi ninakosea kufikiri kuwa Mhimili mmoja unamtumia Mwenyekiti wa chama kuunda mhimili mwingine? Ukishaundwa unaweza kuusimamia mhimili uliohusika kuunda?! La hasha! Hauwezi kukaa kichwani, utakaa mfukoni.

6. Majina ya wabunge waliokatwa, yangekatwa baada ya kura za maoni ya wajumbe si kabla. Sasa yamekatwa na viongozi ambao hawajawahi kuongozwa na wabunge. Wajumbe wakiamua kuwapigia kura hata kama hawamo kwenye orodha, itakuwaje?! Si mnasema mamlaka ni ya wananchi?!

7. Sitashangaa wajumbe wakiwaangusha wengi wabunge waliopenyezwa na Kamati Kuu. Kama wana CCM wanawaangusha wabunge wao, ingekuwaje kama wabunge hao wangepambanishwa na wabunge wa upinzani? Mabunge ya Spika Makinda na Sitta, yanashikilia rekodi isiyovunjwa. Bunge lijalo laweza kuvunja rekodi ya unyenyekevu kwa dola.

8. Ile kauli mbiu ya “vichaa” wa “No Reform, No Election” leo imepata promo. Waliobeza hoja ya mgombea binafsi na hoja ya kupunguza madaraka ya viongozi, leo wameonja matunda ya kubeza. Vyama vinapora uhuru wa watu na kuwageuza watumwa. Vinawanyima wananchi uhuru wa kumchagua wampendaye. Vinataka kura za wasio na vyama lakini hawawezi kupigiwa kura. Piga, ua, HII NI DHAMBI KUBWA. Katiba yetu haimchagulii mtu dini, mke/mme, au aishi wapi LAKINI inamlazimisha mtu awe na chama ili aweze kuongoza hata kijiwe.

9. Watawala wana hofu kubwa dhidi ya wapinzani. Matokeo ya hofu ni kuwavumilia watu hatari ndani ya chama tawala. Mafisadi, magaidi, watekaji, wauza madawa ya kulevya, wahamiaji haramu, mashoga, nk WANAWEZA kuvumiliwa kwa sababu ya hofu ya wapinzani. Midomo ya chama imepigwa kufuli isikemee rushwa. Vikao vya siri vinatumia kigezo cha rushwa kukomoa watu lakini hakuna kiongozi atathubutu kukemea rushwa hadharani.

10. Kwa nia njema, Urais (Presidency) ni mhimili wa nne. Urais unatupatia rais ambaye si binadamu na si Mungu. Matokeo yake, watu wanakamiana na kuumizana juu ya taasisi hii isiyoishi duniani wala mbinguni. Uchaguzi wa 2025 haujafanyika (hata kama matokeo tunayajua), lakini watu tayari wanaumizana kwa uchaguzi wa 2030! Tutampata wapi rais malaika au mwanadamu?

Ukikosa usingizi, jifanye unaomba. Mashaka yakizidi matumaini, machawa wanaongezewa dau; vinginevyo njia ya kwenda chooni inaota magugu.
 
🤣🤣...kuiongoza hii nchi 2025-2030 itakuwa vigumu sana, atakayepewa kuongoza atapata shida sana kuliko hata shida wanazopata wananchi.....huyo kiongozi ajipange kuua sana watu, kuteka sana, kufungua fungia taasisi mbalimbali na watu kufungiwa, atafunga mpaka bagia😄...na hii ni mbinu ya mtu ambaye hana akili hawezi tumia ubongo wake bali nguvu, ndani kutakuwa na moto na nje kutakuwa kunawaka moto😆
 
Vikao vya siri vinatumia kigezo cha rushwa kukomoa watu lakini hakuna kiongozi atathubutu kukemea rushwa hadharani.
 
Hakuna kitu hapa, ameweka makengeza tu hapa anaponda ponda kila kitu..
YEYE ni MUNGU hadi aseme hk ni dhambi kile si dhambi?

akawashauri BAA ya VICHAA huko
 
Hiyo namba tano kama haukusoma civics huwezi kuelewa
 
Your browser is not able to display this video.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…