Askofu Bagonza nauliza upo upande upi kisiasa?

Deogratias Mutungi,

HOJA NZITO na CHAPISHO moto hasa.

KARAGWE Kuna Mambo jamani, si maaskofu wa KKKT si maaskofu wa KATOLIKI.

Naikumbuka Sana misimamo na fikra tunduizi za msomi Padri Privatus Karugendo.

Natamani kujua historia ya ARI YAO katika Vita dhidi ya utumwa,ukoloni na jinsi walivyomuunga mkono mwalimu Nyerere kipindi Cha kudai UHURU.

KARAGWE kuna minyukano jama mara hawa WANA PUA PANA. Mara wale WANA PUA NDEFU MCHONGOKO.

Nasubiri kwa hamu kumuona baba yetu askofu msomi Dr.Bagonza akitujuza vijana wake tuliozaliwa miaka ya kutosha baada ya VITA YA KAGERA.

Hongera sana mtoa hoja!!
 
Ndani ya joho la uaskofu ana kadi ya Chadema
 

Maneno ya watu masikini wa fikra haya.
 
Kama kila anayemsifu Magufuli au anayekosoa upinzani ni ccm hivyo pia kila anayekosoa serikali ni chadema au Act.
 
Kiongozi wadini kujihusisha na siasa ni mwanzo wa kuwagawa wa umini wako na wewe unaanza kuonekana kama mtu wa dunia zaidi siyo wa dini
 
Huyu mleta mada alitakiwa awe na mifano ya hoja zake..kama Hana mana yake kuna upande anautumikia tena kwa fitina. MADA ZOTE ZA BAGONZA. Nyingi ni mada fundisha na mada ama mada onyo..askofu hawezi kutumia fimbo ama lugha hasi kuonya!mchungaji ama askofu hutumia neno Ole kwa watenda mabaya na Kheri kwa wema!
Askofu BAGONZA amatumia fasihi adimu katka makala adimu anazoandoika..Ebu fikilia kilichotokea Malawi!!mtamchukia hyu mtumishi kwasabb njaa always makes people blind believe me..hyu amekua mwalimu mzuri wa nyakati hizi msimchukie ila tumieni Hekima ya uandishi wake!!
Huyu ni mwalimu mzuri wa nyakat hizi tumuunge mkono.
Ameni
 
Huyo ni Chadema na mshauri wa Mbowe
Hizi ndo fikra binafsi zisizo na miguu ya kusimamia,alikuambia ni mshauri wa mbowe!,Mwanadamu unapokosa utashi huweza kufananishwa na chochote hata kitu kisicho na maana kabisa
 
Ndio ni mwanachama wa Chadema na ni mshauri wa Mbowe
Hizi ndo fikra binafsi zisizo na miguu ya kusimamia,alikuambia ni mshauri wa mbowe!,Mwanadamu unapokosa utashi huweza kufananishwa na chochote hata kitu kisicho na maana kabisa
 
Hongera:andiko mujarabu kabisa hili
 
Askofu Dr. Bagonza anasubiriwa kwa hamu na wagosi kule Tanga , aende akakatwe makende, yeye na Askofu Munga wameifilisi Dayosisi vibaya mno.

Akili yako inafikiri kuhusu pesa tu. Hili ni tatizo kwako. Rekebisha...

Hoja iliyoko mezani kwa mujibi was mleta mada ni Askofu Bagonza vs Dini vs Siasa....

Je ni halali kiongozi wa Dini (Askofu, Mchungaji ama Padri nk) kutoa maoni yake yenye mlengo wa kukosoa watawala (wanasiasa)?

Je, huko ni kuchanganya siasa na dini? Je, ni kweli kuwa ili ukosoe watawala/wanasiasa, sharti aidha uamue kuwa mwanasiasa na ujulikane wewe ni member wa chama gani cha siasa kwa mujibu wa mleta mada?

Hiki ulichikiandika ni nje kabisa ya mada...!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…