Hatuhitaji CCM mpya wala CHADEMA mpya, hatuhitaji kaulimbiu mpya. Tunahitaji Tanzania Mpya inayowezesha Raia wake kuishi kwa furaha na watu wasiokubaliana nao.
Kazi ya kujenga Tanzania mpya ni yetu sote mpaka tufikie hatua ambayo...
Simba anaweza kuishi na Yanga kwa furaha,
Chui acheze na mwanambuzi kwa furaha,
Simba amwalike swala katika sherehe,
Mbwa amuuguze sungura anapougua badala ya kumla ,
MwanaCCM amuoe mwanaCHADEMA bila kufikiriwa kwamba anasaliti,
Afande Kingai amwalike Mbowe kwenye Send Off ya mwanaye,
Tanzania ambamo mtoto wa Denice Urio amuoe mtoto wa Kibatala na iwe furaha na vicheko.
huwezi kufika ya mbinguni kama makazi haya tunayoyaishi sasa hatuishi kwa upendo baina yako na mm na mwingine. Kazi ya viongozi wa dini ni kutuelekeza namna bora ya kuishi ili tufike huko unaposema.