Askofu Bagonza: Tusitegemee uwajibika ripoti ya CAG

Askofu Bagonza: Tusitegemee uwajibika ripoti ya CAG

juma30

Senior Member
Joined
Jun 25, 2022
Posts
159
Reaction score
459
ASKOFU Benson Bagonza amesema Rais ni sehemu ya bunge, Bunge haliwezi kuiwajibisha Serikali kwa kuwa Rais ni sehemu ya Bunge.

"Rais ni sehemu ya bunge, Bunge haliwezi kuiwajibisha Serikali kwa kuwa Rais ni sehemu ya bunge, lakini Rais huyo huyo ndiye anayewateua Jaji Mkuu na majaji wengine na hata Mahakama zinamuomba Rais fedha za kufanya shughuli zake, hivyo ni vigumu kuwa na ripoti ya CAG zinazofanyiwa kazi kikamilifu" Askofu Dkt.Benson Bagonza

"Katika Taifa letu nimegundua hatuna kitu kinachoaitwa Separation of powers (mgawanyo wa madaraka), kwamba Bunge, Serikali na Mahakama zinafanya kazi independently (zikijitegemea) Nachikiona ni kama tuna hangover (mning'nio) ya kutoka chama kimoja, tulitoka chama kimoja lakini kimsingi bado mambo yote yamekaa kichama kimoja kwamba Bunge, Serikali hata pengine mahakama ni mali ya chama" Askofu Dkt. Benson Bagonza
 
Tungetawaliwa na mjerumani au mwingereza tusingekuwa hivi tulivyo, tungechangamka na hizo pesa zetu tungezichimba kwenye mijengo yao inayochipua uswahilini kwetu.
 
Ngonjera za CAG hizo anaimba kila mwaka, zaidi anaitia aibu sirikali
 
Mbunge alitakiwa achangiwe posho za kutekeleza majukumu yake ya kibunge na wananchi anaowawakilisha jimboni kwake, hii ya serikali kumlipa mbunge mshahara, posho na marupurupu hiyo tayari ni rushwa kwa mbunge, wataishia tu kusema ndiyooooooooooo kwa hoja yoyote ya serikali.......
 
Wananchi tutadanganywa mpaka lini? Ifike mahali tuseme baaaaaaasi!! enough is enough.
 
CCM ni genge la majizi yanayopokezana vijiti ili yaendelee kutuibia. Vijana amkeni mfanye mapinduzi vinginevyo mtaendelea kusindikiza watoto wa mafisadi
 
Tuko buzzy na kupinga Ushoga na usagaji, report ya CAG sio kipaumbele chetu.

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Askofu amegundua sasa. ?!! Watu wanaodai Katiba mpya wanajua habari hiyo ya separation of power kitambo sana !!

Bado tupo mbali sana !! Lakini Mungu si Asumani !!
 
Tuko buzzy na kupinga Ushoga na usagaji, report ya CAG sio kipaumbele chetu.

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Hiyo habari ya Ushoga ni ujinga ulioanzishwa ili kuwasahaulisha watu report ya CAG !! Tupo mbali sana na tumelala fofofo hatujitambui !!
 
Back
Top Bottom