Inside10
JF-Expert Member
- May 20, 2011
- 29,909
- 32,414
UKIISHI MUDA MREFU UNAWAONA MWAMBUKUSI WENGI…
Wanyambo wenye hekima husema, “Bora uporwe mali kuliko kuzeeka, kwa sababu ukiporwa mali, marafiki zako wanaweza kukuchangia ukawa na mali tena”.
Mimi sasa ni mzee na nimewahi kuona “Vi-Mwambukusi” na “Ma-Mwambukusi wengi”. Nitaje?
1. Nilimwona Kambarage. Waingereza “wakamMwambukusi” kuwa ni mchochezi. Akahukumiwa. Faini ikalipwa. Ikawa jioni, ikawa asubuhi, akawa rais wetu. Waingereza wakapiga saluti, bendera yao ikashuka, ya “Mwambukusi” ikapanda.
2. Nilimwona Madiba Mandela. Makaburu “WakamMwambukusi” kuwa ni gaidi. Miaka 27 akanyea debe, na alipoomba maji ya kunywa, Askari jela alimpa mkojo wake anywe. Ikawa jioni, ikawa asubuhi. Mandela akawa Rais. Akakutana na Askari aliyempa mkojo. Akamkaribisha mezani kula naye. Askari akatokwa na jasho katikati ya baridi kali.
3. Kuna mmoja simtaji jina. Akakamatwa na polisi wa barabarani. Akabambikiwa makosa ya usalama barabarani. Akapewa kebehi. Akaambiwa ang’atwe na mbu kwa kuwa mbu wana haki ya kupata chakula. Leo ni rais wao. Askari wanampigia saluti. Akisinzia ndani wanalala nje kumlinda. Akikooa, wanampongeza kwa afya njema. Hicho ndicho kisasi bora kuliko vyote.
Namwamini Yesu Kristo. WalimMwambukusi mpaka kaburini. Akafufuka, wakamsujudia na kuishi naye.
Mitume wote, manabii wote - hakuna aliyeepuka uMwambukusi. Achana na hawa mitume wetu wasiotumwa na yeyote. Puuza hawa manabii wetu wasio na unabii bali wamejawa na uhitaji.
Sasa Mwambukusi ndiyo habari ya mjini. Si wa kwanza kuwa rais wa TLS na si wa mwisho. Nampongeza. Nina neno naye. Asiogope kujaribu kutikisa mbuyu lakini pia asiogope kushindwa. Kwa nini? Waliomtesa ndio wahanga wa kesho wa mfumo ule ule.
Katika enzi hizi ni “Ni hatari kuwa sahihi wakati serikali imekosea”. Bora ukosee wakati serikali iko sahihi.
Penye haki wote tuko salama. Penye dhuluma hakuna aliye salama. Asubuhi waweza kupigiwa makofi na saluti; jioni ukapigwa makofi na kurushwa kichura.
Nyerere alimwambia Mandela alipokuja Tanzania. “You are not free; you are out of jail”. Mfumo ni kitu cha hatari. Kina tabia ya kuwala hata waliokiunda.
Msimuharibie Mwambukusi. Namwona ana uwezo wa kujiharibia. Leo twampenda sote; kuna siku tutamchukia wote. Hakuna umaarufu wa kudumu. Inayodumu ni haki.
Kwetu sote wana na mabinti wa Tanzania, tupendane.