Sawa kabisa Askofu,ccm wanatumia maji ya pilipili halafu wanakimbilia ulipo mchanga,sasa kinachotokea baada ya hapo ni vumbi kutimka!Huwa wanafanya nini mimi sijui,labda ajitokeze mwana ccm mmoja aseme wasiseme tunawasemea.Karibu namaliza mwaka 1 nikiwa Mwalimu wa Chuo Kikuu. Kimsingi, kila Askofu ni Mwalimu lakini si kila Mwalimu ni Askofu. Kwa bahati mbaya nina vyote! Tangu Septemba 2025 nafundisha somo la POLITICAL PHILOSOPY kwa wanafunzi wanaosoma Sayansi ya Siasa.
Hapa mezani kwangu, nina nyaraka za Maridhiano ya nchi za Afrika ya Kusini, Rwanda, Kenya, Sierra Leone, Gambia na Cyprus.
Kila nchi ina mazingira yake, lakini maridhiano ni suala linalohitajika endapo “jambo kubwa lisilo la kawaida” limetokea na kuigawa nchi kwa vitendo vyenye sura ya JINAI KUBWA ambavyo hata vikinyamaziwa, vitakwamisha ustawi wa taifa husika.
Ziko faida 4 za maridhiano bila kujali nchi iko wapi na ina historia gani:
1. Ni njia ya kuanza upya baada ya kukosea. Unakiri na kuomba kuanza upya.
2. Ni kujifunza “kushindwa” na sauti inayodai uwajibikaji wa kijamii. Unakubali kushindwa hata kama unaamini umeshinda.
3. Ni njia kuzuia “ufukuaji wa makaburi” hapo baadaye. Hili ni muhimu sana hata ndani ya vyama na serikali tawala kuliko vyama pinzani. Bila hatua hii, watu hugeuza historia kuwa agenda ya kisiasa.
4. Ni njia ya kuwatoa kifungoni watawala na kuwarejeshea mamlaka ya kimaadili (Moral authority). Hii ni kuweka silaha chini na kuongoza kwa ushawishi. Wananchi walionuna wana nguvu kuliko maandamano.
MUHIMU
Nyaraka zote nilizo nazo zinasisitiza ulazima na umuhimu wa maridhiano na kwamba, “Usimwache nje mtu au kundi lolote lenye ushawishi, ambalo linaweza kurudisha nyuma mapatano yote yaliyofikiwa wakati limeachwa nje”.
Ushawishi una nguvu kuliko silaha. Mwenye silaha hujaa kiburi wakati mwenye hushawishi hutumia akili na hekima.
Mjaluo mmoja ameniambia kuwa kuchelewesha msawaaridhiano ya KWELI ni sawa na kuchambia maji ya pilipili🤣🤣.
Akaongeza, ujanja ujanja hautakiwi katika maridhiano.
Sijui amejuaje wakati Wajaluo wakimaliza huwa wanaenda ziwani kuogelea🤷🤷🤷🤷
TUNAELEKEA KUCHELEWA. Ndevu zikiishaota hazirudi ndani.
1,2,4 hawataki hata kuzisikia 📌Karibu namaliza mwaka 1 nikiwa Mwalimu wa Chuo Kikuu. Kimsingi, kila Askofu ni Mwalimu lakini si kila Mwalimu ni Askofu. Kwa bahati mbaya nina vyote! Tangu Septemba 2025 nafundisha somo la POLITICAL PHILOSOPY kwa wanafunzi wanaosoma Sayansi ya Siasa.
Hapa mezani kwangu, nina nyaraka za Maridhiano ya nchi za Afrika ya Kusini, Rwanda, Kenya, Sierra Leone, Gambia na Cyprus.
Kila nchi ina mazingira yake, lakini maridhiano ni suala linalohitajika endapo “jambo kubwa lisilo la kawaida” limetokea na kuigawa nchi kwa vitendo vyenye sura ya JINAI KUBWA ambavyo hata vikinyamaziwa, vitakwamisha ustawi wa taifa husika.
Ziko faida 4 za maridhiano bila kujali nchi iko wapi na ina historia gani:
1. Ni njia ya kuanza upya baada ya kukosea. Unakiri na kuomba kuanza upya.
2. Ni kujifunza “kushindwa” na sauti inayodai uwajibikaji wa kijamii. Unakubali kushindwa hata kama unaamini umeshinda.
3. Ni njia kuzuia “ufukuaji wa makaburi” hapo baadaye. Hili ni muhimu sana hata ndani ya vyama na serikali tawala kuliko vyama pinzani. Bila hatua hii, watu hugeuza historia kuwa agenda ya kisiasa.
4. Ni njia ya kuwatoa kifungoni watawala na kuwarejeshea mamlaka ya kimaadili (Moral authority). Hii ni kuweka silaha chini na kuongoza kwa ushawishi. Wananchi walionuna wana nguvu kuliko maandamano.
MUHIMU
Nyaraka zote nilizo nazo zinasisitiza ulazima na umuhimu wa maridhiano na kwamba, “Usimwache nje mtu au kundi lolote lenye ushawishi, ambalo linaweza kurudisha nyuma mapatano yote yaliyofikiwa wakati limeachwa nje”.
Ushawishi una nguvu kuliko silaha. Mwenye silaha hujaa kiburi wakati mwenye hushawishi hutumia akili na hekima.
Mjaluo mmoja ameniambia kuwa kuchelewesha maridhiano ya KWELI ni sawa na kuchambia maji ya pilipili🤣🤣.