Sakata la Ngorongoro/Loliondo ni darasa maalum kwa tasnia mtambuka. Waweza kuchagua mkondo gani wa darasa uingie kujifunza.
1. Habari/Media.
Tulizoea tasnia hii ikirukia kuandika habari hata ikiwa na robo ya ukweli. Kwa kawaida, hawa jamaa kwa kukimbizana na ushindani, huwa wanapakua chakula kibichi. Hivi sasa wana ukweli wote lakini hawaandiki.
2. Uongozi/Utawala
Tumezoea kuona viongozi wenye uwezo wa kubadilika na kuwa watawala au watawala wanaoweza kubadilika na kuwa viongozi.
Sakata hili limekataa utawala. Linataka uongozi tu.
3. Diplomasia ya Kimataifa
Tumezoea kuona wizara inayohusika na masuala ya kidiplomasia ikisikika pale suala lolote linapogusa nchi zaidi ya moja. Safari hii tunaona "diplomasia kimya" katikati ya kelele za nchi mbili.
4. Haki za Binadamu na Wanyama
Tulizoea kuona haki za binadamu hazilinganishwi na kitu chochote. Safari hii tuna sylabus mpya. Haki za binadamu zinaishia pale haki za wanyama zinapoanzia. Na zote mbili zinaishia pale haki za mazingira zinapoanzia.
Na zote tatu zinaishia pale haki za tumbo zinapoanzia. Ukichelewa kufa unayaona haya.
5. Royal Tour na Roho Tua.
Royal Tour yakaribisha wageni. Nyumba yenye kelele hukimbiwa na wageni, si kutembelewa. Ukikimbia kelele unatafuta pa Kutua Roho yako. Jirani akiachia kuku wake bila utaratibu, mayai watataga kwa jirani.
Jirani wapendane au wachukiane, wakizaa watoto wanaofanana ni darasa kama la Ngorongoro-Loliondo.
Tusitafute mshindi. Tufute mchezo tuanze upya. Kocha yule yule, kapteni tofauti, wachezaji wale wale Washangiliaji wale wale ila wanyanganywe viroba wapewe mavuvuzera ya kutosha.
Wanyama watafurahi
Watu watafurahi
Jirani watafurahi
Wageni watafurahi
Mazingira yatafurahi
HEKIMA UHURU NA UMOJA.