Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Akizungumza hii leo na waandishi wa habari kuhusiana na zoezi la Uchaguzi wa Serikali za Mitaa linaloendelea nchini, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) na Askofu Mkuu wa Dayosisi ya Kaskazini ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Fredrick Shoo ameitaka serikali na wasimamizi wa uchaguzi kufanya kazi kwa uadilifu na bila upendeleo wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa.
Soma: Askofu Fredrick Shoo alia na rafu zinazoendelea kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Ataja mbinu zinazotumika kuengua Wagombea!