Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Akizungumza kwa niaba ya Baraza la Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), Askofu Mkuu wa Dayosisi ya Kaskazini ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dkt. Fredrick Shoo, ametoa wito kwa mamlaka na vyombo vyote vinavyohusika kuhakikisha vyama vyote vya siasa vinavyogombea uchaguzi wa serikali za mitaa vinapata fursa sawa ya kufanya mikutano yao kwa uhuru na usawa, bila bugudha au kubaguliwa.
Pia, Soma: Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) watoa wito wananchi kushiriki uchaguzi serikali za mitaa
Dkt. Shoo alisisitiza kuwa ni muhimu kwamba vyama vya siasa vikatekeleza kampeni zao katika mazingira ya usawa, bila kushinikizwa au kuelezwa mipaka isiyo ya haki, huku akisisitiza kuwa ni haki ya kila chama kufanya kampeni bila kuingiliwa "Mamlaka zinatakiwa kutoa wigo sawa kwa vyama vyote vya siasa kufanya mikutano yao, kufanya mikutano yao kwa uhuru na usawa bila bugudha au kubaguliwa"