Uchaguzi 2020 Askofu Gwajima ameonesha njia, wanaompinga hawana hoja

Gwajima kuiteka kawe ni lazima . Huyu gwajim Namsikiaga tuu ila hekima yake inatosha kuongoza
 
Kama.hana madhara mbona mnatoa milio Sana kana kwamba ametangaza pekeake kugombea nchi nzima

Afu nimekuta tu hii mada sina hata muda kujua mambo ya watu gani wanagombea wapi after all kwa case ya Gwaji boy wala sina tatizo nae dunia yangu na yake ni mbali mbali ila tu namchukulia kama mtu ambae maadili yake na wafuasi alio nao ni kielelezo cha kiwango na ufahamu wa jamii tunawakubali sana watu tukihisi ni sahihi lkn sio ki hivyo na hapa tatizo ni jamii sio ‘opportunist’

Tuna safari
 
Mungu ni mwema Sana, hata CCM wasipo mpa nafasi. Mungu anaweza fanya njia akapata moja wapo ya nafasi ya ubunge wa kuteuliwa. Mtu wa Mungu yule akitinga pale mjengoni patanoga Sana.
 
Nikwambie kitu?
Umetumia nguvu kubwa sana kumkampenia huyu bwana, ndiyo maana imepelekea watu wahisi wewe ndiye gwajiboy mwenyewe unayejikakamua kujivua gamba!

Una point zilizo wazi sana lakini habari umeiprolong hadi imejaa kitabu, inechusha!

Sasa utetezi wako ungelijenga pia hoja ya kumsafisha kwa ukengeufu wake wa kimaadili kuzini na malaya na kujirekodi kisha kujipost.

Hilo ndiyo ungelikazia sana, kwa sababu viongozi wa kitaifa hawatakiwi kuwa wahunihuni,maana ni vioo vya jamii, ndiyo maana ya kuchunguza vyote hivyo.

Gwajiboy akiingia 'kilingeni' atawatoa kamasi sana ninajua, lakini kipindi hiki jaribu sasa kumsafisha vizuri ili aingiapo mjengoni watu wasimbeze kila mara 'atemapo madini'kwa ku attach clip yake ya ngono uzembe.
 
Uzuri sasa hivi upinzani umehamia ndani ya ccm, so tusubiri watia nis wengine ndani ya ccm jimbo la kawe tuwapime
 
Hahahaha gwaji boy ni msanii sababu ameamua kuingia katika list ya wasanii wenzie
 
Hiyo clip ndio silaha yenu ya mwisho si ndio? Basi nawaambia mmeshafeli hadi hapo
 
Askofu ni mtu wa misimamo sana. Tunahitaji viongozi wa namna yake ili kuikomboa nchi yetu. Nafikiri watu wa kawe wamepata bahati, wenye ufahamu mzuri wanaelewa hii nchi ilikotoka na namna ambayo Askofu Gwajima amekuwa mstari wa mbele kunyosha palipopindishwa. Huu ni wakati wa yeye kuwepo katika siasa ili aiathiri kwa namna chanya. Big up bishop Gwajima
 
Ishu siyo Uaskofu wake, ishu ni maadili, kiongozi lazima uwe mfano kwa unaowaongoza. Ile video yake pendwa imemtia doa kubwa sana, na yale matusi aliyomporomoshea Cardinal Pengo ndiyo kabisa yamemuondolea sifa ya kuwa kiongozi,na kwa maneno yake mwenyewe ni kuwa kumtukana mtumishi wa Mungu ni kujitakia laana,hivyo tayari alipo hapo anatembea na laana ya kumtukana Cardinal Pengo.
Your browser is not able to display this video.
 
Mungu ni mwema Sana, hata CCM wasipo mpa nafasi. Mungu anaweza fanya njia akapata moja wapo ya nafasi ya ubunge wa kuteuliwa. Mtu wa Mungu yule akitinga pale mjengoni patanoga Sana.
Ubunge wa vitu maalum
 
Ni haki yake kikatiba apewe nafasi. Jambo jema kwake ni kwamba, anagombe ubunge kupitia chama cha mapinduzi chama ambacho kinajipambanua kwa kutetea wanyonge.
Ila kura zisiibiwe maana atageuka kuwa mtumishi wa shetani, maana shetani ni mwizi.
 
Angefaa kwenye siasa za nchi zilizostaarabika sio Tanzania. Unakuwaje upande wa serikali isiyofuata misingi ya demokrasia na utawala bora, kama kupiga marufuku watu wasitumie haki zao za kikatiba kufanya siasa za hadhara, kuteka watu na kuendesha siasa za kiimla.

Ina maana Gwajima anapendezwa sana na siasa za mrengo huo mpaka ameamua awe part and percel ya mfumo huo kandamizi?
 
Ana haki kugombea ni sawa.
Ila sio mtu wa maadili kama anavyotaka aonekane!
Sio nabii wa Mungu hata kdg bali alichofanya ni kama wale waganga wa kienyeji wanaojipa majina ili kufanikisha 'azma' yao.
hakuna uponyaji au miujiza hata chembe kama anavyojinasibu.
Wajinga ndio waliwao
 
Wanasema elimu haina mwisho. Hivi jamani ukiwa mchungaji ni lazima uwe na sifa ya uwongo? Sasa hapa kweli kuna mtu kampinga Gwajima kutia nia kwasababu za kuchanganya dini na siasa? Au sababu hii imetungwa tu kuhalalisha hiyo kampeni. Mie ninachokumbuka ni kuwa wtu wanahoji imekuwaje huyu bwana mkubwa wa anfifilo ayageuke maneno yake ya kuwa yeye ni mtumishi wa Mungu aliye hai na ni cheo kikubwa kuliko uwaziri na hata uraisi. Hakuna hata mmoja anayesema ni mwiko kuchanganya siasa na dini bali ni hoja ya kutungwa ili ionekane anapingwa kwa uonevu.
 
Hiyo clip ndio silaha yenu ya mwisho si ndio? Basi nawaambia mmeshafeli hadi hapo
Haukunisoma kwa makini, nipo upande wako na Gwajiboy ninampenda, isipokuwa wewe 'classmet' wake unamsifia bila kumsafisha, ndiyo nikakukumbusha hilo.

Kwa kuwa ushafunga uzi? Anzisha thread nyingine umsafishe kabisa umuondolee udhu.

Tunajua kakifika mjengoni ni 'kadume' katawachachafya ad watalia poooh'
 
Gwaji boy ni mtu wa amsha amsha angekuwa kwenye jimbo langu lazima ningempa kura yangu bila kujali chama gani anagombea.
 
Hivi kuna mtu ana hofu na Gwajima kugombea ubunge?

Sijui kama kuna watu atawahadaa kama anavyowahadaa wafuasi wake kuwa yeye ni mtumishi wa Mungu.

Utapeli mkubwa wa zama hizi ni kupitia maneno ya Mungu. Gwajima ni miongoni mwa wanaoitumia biblia kutekeleza uovu wake. Kanisani kwake, kidogo kidogo, wafuasi wake wanapatwa na utambuzi. Hali hiyo imemfanya atafute mbinu mpya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…