HaMachiach
JF-Expert Member
- Dec 15, 2015
- 3,417
- 6,149
Dar es Salaam
Wakati chanjo za UVIKO-19 tayari zipo nchini, na tayari watu wanafanya uamuzi wa kuchanjwa au kutochanjwa, zimekuwepo kauli mbali mbali kuhusu umuhimu wa kuchanjwa au kutochanjwa.
Ikumbukwe kuwa rais Samia baada ya kuchukua hatamu, alisema kuwa atapata ushauri wa wataalamu kuhusu maswala yahusuyo UVIKO-19 kwa sababu ni janga la kimataifa. Katika kutekeleza hilo, rais aliunda kamati ya watalaamu, ambao baada ya kumaliza utafiti wao pamoja na mambo mengine waliyoshauri walisema chanjo iruhusiwe lakini iwe ya hiari.
Ikumbukwe kwamba UVIKO-19 iliingia nchini mwaka jana mwezi Machi kupitia mgonjwa aliyegundulika kule Arusha. Mbali na kuwepo na presha za kimataifa za kutangaza idadi za wagonjwa na kufungia watu ndani, Tanzania ilichukua msimamo wa kutofungia watu ndani, huku hayati Magufuli akiwaondoa watu hofu. Msimamo wa hayati Magufuli ndo uliolibeba taifa wakati majirani zetu Kenya na Uganda wakijifungia ndani. Wakati Kenya na Uganda wakitangaza idadi ya wagonjwa kuongezeka, watanzania waliendelea kufanya kazi zao lakini wakishauriwa kuchukua tahadhali. Ilifikia wakati maisha yakawa kawaida na hofu ikawa imeondoka.
Nyote mnajua kuwa kampeni za uchaguzi zilizokusanya watu wengi zilizifanyika na hakukuwa na madhala yote. Ilikuwepo pia mikusanyiko mingine ya watu wengi mfano kwenye mazishi ya hayati Magufuli, na mechi za soka ambavyo kama UVIKO-19 ingekuwa inaenea kupitia mikusanyiko basi madhara yangekuwa makubwa. Yamkini ilienea kwa watu, na watu wameishatengeneza kinga ya asili.
Rais Samia kwa busara zake, kwa kuangalia uhitaji wa makundi mbali mbali, ameona ni sawa chanjo ikiruhusiwa ila tu iwe ya hiari. Gwajima amempongeza rais kuhusu maamuzi haya maana kuna wanaohitaji chanjo wakidhi masharti ya kusafiri kama kwenda hija au kwa safari za kibiashara. Kwa kuangalia makundi haya, uhalali wa kuruhusu chanjo iwe ya hiari ni sawa ili yule anayetaka achanjwe.
Ikumbukwe yamekuwepo makundi yanayomshtumu rais kwamba ameruhusu chanjo. Makundi haya yamemshutumu kwa sababu amechukua mlengo tofauti na hayati Magufuli. Ifahamike kwamba pamoja na kwamba Magufuli alilivusha taifa katika kipindi kigumu, kwa sasa ni wakati wa rais Samia, hatuna budi kusimama naye. Mbali na hilo, rais Samia amezingatia haki ya kikatiba ya raia kwamba wanayo haki ya kuchagua wanayoyataka lakini pia haki ya kuabudu, na haki ya kusafiri ambazo kama kutochanjwa ni kikwazo wangekosa haki hizi. Kama wakikosa basi iwe ni hiari yao, na rais ameona vyema wanaotaka kuchanjwa wachanjwe kutimiza haja zao.
Lakini pia UVIKO-19 sio suala la Tanzania peke yake, ni swala la kimataifa kwa hiyo ni muhimu kulilinda taifa na watu wake katika medani za kimataifa liendelee kuwa salama na uchumi wake kuwa imara.
Ni kwa mlengo huo sasa, pamoja na mambo mengine, Askofu Dr Gwajima ambaye ni mbunge wa Kawe amesema uamuzi wa rais Samia wa kuruhusu chanjo iwe ya hiari uko sawa.
Na mimi kama mwananchi wa Kawe nampongeza mbunge wangu Gwajima kwa kusimama na rais.
Said Shabani
Mpobo - Madale.
shabanis@gmail.com