#COVID19 Askofu Gwajima: Chanjo ya Corona ni hatari, ni chapa ya mpinga Kristo, Mataifa kututenga kwa sababu hatujachanjwa ni mwanzo wa Uchumi wetu kukua

Cannabis

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2014
Posts
11,557
Reaction score
33,535
Askofu Gwajima ameonya waumini wake kwamba chanjo ya corona ni hatari, na kusisitiza hakuna haja ya kuchanja watanzania kwa sababu Tanzania hakuna corona. Askofu Gwajima amesema kilichopo hivi sasa ni hofu ya corona ambayo ina nguvu kuliko corona yenyewe.

Askofu Gwajima amesema kwamba chanjo ya corona inageuza mwanadamu kuwa mwandamu wa aina nyingine, kwamba chanjo hiyo inakubadilisha uwezo wa kufikiri, hisia na maamuzi.

Amesema kwamba Tanzania itakapotengwa kwa kugoma kuchanjwa ndio itakuwa mwanzo wa Tanzania kuwa na uchumi mkubwa duniani, amesema hiyo itasababishwa na wazungu mabilionea wenye akili watakogundua kuwa kuna taifa moja pekee ambalo halichanji watu wake na hivyo wazungu hao mabilionea watakuja na kuanza maisha yao nchini Tanzania na kuhamishia biashara zao kubwa nchini Tanzania.

Amesisitiza kuwa alipata maono miaka 25 iliyopita kuwa wazungu wengi watakuwa ubalozi wa Tanzania wakifurika kuomba visa ya kuja kuishi Tanzania.

Askofu Gwajima amesali na kuomba serikali na viongozi wa Tanzania wagome kuchanja watu kwa maana ndio itakuwa mwanzo wa Tanzania kuwa na uchumi imara.


 
Mi mtu yeyote akija na mambo kama haya mi simsikilizi kabisa, maradhi na jinsi ya kujikinga ni masuala ya kitaalamu. Wana taaluma ndio wa kutoa miongozo nini cha kufanyika, kuwaambia watu waamini vitu ambavyo wewe mwenyewe huvijui ni kuwaona hawana akili au mazoba.

Miaka na miaka,vizazi na vizazi watu huomba dua kwa M/Mungu awatolee maradhi, dawa zikipatikana mi naamini ni mojawapo ya majibu ya dua zetu,sasa iwapo dawa za ugonjwa zipo alafu unazizadharau naona ni udhaifu wa fikra.

Ugonjwa wa Polio umemalizika sehemu nyingi duniani kutokana na chanjo ya hao wanaoitwa mabeberu, lakini nchi za Afghanistan, Nigeria na Pakistan bado upo sababu watu wanaaminishwa na viongozi wao kuwa wazungu wanataka kuwauwa na kuwatia maradhi.
 
Wazungu wa USA wangetoa haraka majina ya watu waliowapiga ban. Kwa mhemo wa pumzi ya CHID BOY unaweza kukuta yupo katika wale walaghai wa uchaguzi mkuu.
 
Huyu ni askofu au tapeli?

WHO wanathibitisha viwango vya utafiti wa dawa, ufanisi wa dawa, na kuratibu madhara wkt wa matumizi.

Huyo askofu anatoa maamuzi kuipinga WHO.

madhara ya kutopata chanjo ni kuzuiwa raia wa Tz kuingia nchi zilizochanja watu wake Hadi Apate chanjo.

Bidhaa za Tz zitazuiwa kimataifa. Sababu zinaweza kubeba virus vya Corona. Rejea upatikanaji wA hivyo virus ktk mbuzi na mapapai.

Nchi itakuwa na Hali ngumu kwa kutengwa na nchi zingine.
 
Siku gwajiboy akiuuza mali zake zote na kuwagawia masikini ndo nitajua anauutimiza unabii.Ila waumini wake walivyo watakubali na kuamini hayo anayoyasema.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…