Jidu La Mabambasi
JF-Expert Member
- Oct 20, 2014
- 16,419
- 26,594
Mategemeo ya wana Kawe kuwa wamepata mkombozi atakayewatetea juu ya kero za jimbo la Kawe zimeanza kuporomoka kwa kasi ya ajabu.
Wengine wanasemma kawe tuna mkosi , katika kupata wabunge wa kututetea.
Wana Kawe wengi wanajiuliza Askofu Gwajima ataingia ofisi ipi ya serikali kuipiia magoti ili kero za wana Kawe zitatuliwe.
Kuna kero kuu za :
- Barabara-ukilinganisha na wilaya nyngine za DSM Kawe iko nyuma sana. Miradi ya barabara ni kama hakuna, leo nenda Kijichi na mtu unajionea kile serikali imewekeza kwa makazi huko.
- Hospitali kubwa Kawe-kwa sasa hospitali kubwa za kutegemewa Kawe ni kama hakuna. Ugomvi wa Askofu na "mke" wao, Dorothy Gwajima unaleta ukakasi mkubwa kattika ushirikiano wa kupata hospitali kubwa aeneo ya Mbezi, Bunju. Mbweni au Tegeta.
- Uendelezaji wa maeneo ya wazi, michezo na kwa ujumla upendezeshaji wa eneo lote la Kawe, ndio kwa heri. Uwanja wa Tanganyika Packers unabaki kuwa magofu ya kutisha kwa miaka nenda rudi.
Kiujumla tulichotegemea toka kwa Askofu Gwajima ni kama tumelamba kadi gharasha badala ya kadi turufu.