Askofu Gwajima na Jerry Silaa wasimamishwa Ujumbe wa Kamati ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge

Askofu Gwajima na Jerry Silaa wasimamishwa Ujumbe wa Kamati ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge

Linguistic

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2021
Posts
3,669
Reaction score
8,268
Wakuu Wabunge Josephat Gwajima (CCM, Kawe) na Jerry Silaa (CCM, Ukonga) ambao ni wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge wameondolewa kwenye kamati hiyo hadi itakapoamuliwa vinginevyo.

1F914531-E5B6-43FD-898A-4207B3E9FCE1.jpeg


Nini Kitatokea mbeleni Tungoje, Kwa Mtindo Huu Wanaweza Hata Kupewa Adhabu ya kufungiwa wasihudhurie Vikao Vi3 Vya Bunge.

Yetu Macho
 
Bunge limemuondoa mbunge wa Kawe Mh. Josephat Gwajima na yule wa Ukonga Mh Jerry Slaa kutoka kwenye kamati ya haki, maadili na madaraka ya bunge ambako walikuwa ni wajumbe wa kamati.

Kumbe ndio maana askofu Gwajima alijiamini "mno" kumbe alikuwa anacheza uwanja wa nyumbani.

Mungu ni mwema wakati wote!
 
Ubaya wa Dhambi ukiitenda siku hizi haukawii kuilipa. Bahati mbaya watu hawajifunzi. Kwasasa Hawa hawa wenzetu kwenye chama chetu migogoro, minyukano na Kushtakiana ni wao kwa wao.

Tukubaliane nchi yetu wote kila mtu apate anachostahiki sio kupendelewa.
 
Kwa hapa serikali ama bunge limeshinda kwa nguvu Sana na Gwajima amekosa nguvu. Kwann? Kwasbb Gwajima baada ya hukum ya bunge iwe negative au positive ndo kwanzaaa angepata chati maana yeye alisema kwenye zogo ndo pakeee sasa HV atakosa Cha kusema zaidi ya kujiona mshindi
 
Hivi hawa wabunge si ndio watunga sheria? wanashindwa kuelewa principle rahisi na ya msingi ya haki ya NEMO JUDEX IN CAUSA SUA?
 
Back
Top Bottom