Askofu Kakobe vs TRA ndani ya mahakama

Askofu Kakobe vs TRA ndani ya mahakama

Mtini

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2011
Posts
1,492
Reaction score
2,361
Kesi ya askofu kakobe na TRA itakavyokuwa mahakamani.

WAKILI---- Shahidi wewe ni kamishna wa TRA?

SHAHIDI ---Ndiyo.

WAKILI---Ni kitu gani kilifanya muanze kufuatilia ulipaji kodi wa askofu kakobe?

SHAHIDI---Tulianza kufuatilia ulipaji kodi wa kakobe siku ile aliposema ana pesa kuliko serikali.

WAKILI---Ni kosa kusema kuwa una pesa kuliko serikali?

SHAHIDI---Hapana.

WAKILI---Je kuna sheria yoyote inayokataza mtu kumiliki pesa kuliko serikali?

SHAHIDI----Hapana

WAKILI----Ulishawahi kuwa mnafiki?

SHAHIDI ---Hapana

WAKILI---Ulishawahi kujipendekeza kwa wakubwa zako kazini?

SHAHIDI----kimyaa

WAKILI---Jibu mheshimiwa hakimu anakusubilia aandike jibu lako.

SHAHIDI---Sikumbuki,,

WAKILI-----Kakobe alipokuambia ana pesa kuliko serikali wewe ulijua serikali gani?

SHAHIDI---Serikali kuu ya nchi inayoongozwa na mtukufu rais?

WAKILI----Je katika maneno ya askofu kakobe kuna sehemu yoyote kuna maneno uliyoyataja wewe ya (SERIKALI YA MTUKUFU RAIS)

SHAHIDI---Hapana

WAKILI----Sasa kama kama hapana kwa nini wewe unataka kumuongezea maneno askofu kakobe?

SHAHIDI----Simuongezei ila nilikuwa nahisi alimaanisha serikali hii inayoongozwa na mtukufu.

WAKILI---Unakubaliana na mimi kuwa mahakama haiamini katika ushahidi wa kuhisi?

SHAHIDI---sijui

WAKILI ---Kakobe akija hapa na akaisibitishia mahakama kuwa yeye aliposema ana pesa kuliko serikali alimaanisha yeye ana pesa kuliko serikali ya mtaa au kijiji, je utakubaliana na mimi kuwa ulikurupuka kumshtaki kakobe?

SHAHIDI---Kimyaaa

WAKILI-----Unakubaliana na mimi kuwa maisha ya askofu kakobe yanaendeshwa na sadaka za waumini wake kwa kuwa kazi yake ya kila siku nikuwahudumia kiroho waumini wake?

SHAHIDI-----Ndiyo

WAKILI------Unafahamu askofu kakobe ana makanisa mangapi africa na america?

SHAHIDI-----Sijuii

WAKILI -----Unafahamu askofu kakobe ana waumini wangapi africa na america?

SHAHIDI-----Sijui

WAKILI-------Unafahamu kakobe anaingiza sadaka kiasi gani kutoka waumini wake hapa africa na america?

SHAHIDI-----Sijui

WAKILI-----Je kuna sheria yoyote iliyotungwa na bunge au chombo chochote chenye mamlaka inayotaka sadaka zikatwe kodi?

SHAHIDI-----Hakuna.

WAKILI------sasa ni kodi gani mnafuatilia kwa askofu kakobe kama sadaka hazitozwi kodi?wala hujui idadi ya waumini na sadaka anazopata kutoka kwa waumini wake?

SHAHIDI----Kimyaaaaa

Aise kesi itakuwa tamu sana ikifika mahakamani na mimi napenda ifike mahakamani ili watu wasiompenda kakobe waumbuke.

Kesho jumapili tukutane kwenye makanisa ya kakobe yaliyotapakaa nchi nzima tukatoe fungu la kumi na sadaka zingine kuunga mkono kazi nzuri ya MUNGU anayoifanya hapa kwetu.Hakika askofu kakobe ni mpaka mafuta wa bwana ubarikiwe mtumishi wa MUNGU.

Mdude nyagali
sumu ya nyigu-freedom fighter
 
TRA hawahitaji ruhusa ya mahakama ili wamkague au wamhesabie mtu kodi kama ndio hivyo wenye maduka wasingekuwa wanafuatiliwa na maofisa wa TRA

Iwe kamaanisha au hajamaanisha TRA wakitaka wakufuatilie kama wewe ni mlipaji wa kodi mahakama haiwezi kufanya chochote
 
Sadaka ina kodi?
 
Sasa kama hana biashara yoyote watafuatilia wapi?
 
mawakili mmekaa kutetea ujinga tu!! Hivi nyinyi hamna mawazo yoyote ya kumshauri rais Kuhusu maendeleo ya nchi yetu
 
Sasa kama hana biashara yoyote watafuatilia wapi?
Ndio maana ukaambiwa ameitwa kuhojiwa ,kama ulimsikiliza vizuri yule kamishna hayo unayoyasema aliyefafanua

Kama ni sadaka au laa
 
TRA hawahitaji ruhusa ya mahakama ili wamkague au wamhesabie mtu kodi kama ndio hivyo wenye maduka wasingekuwa wanafuatiliwa na maofisa wa TRA

Iwe kamaanisha au hajamaanisha TRA wakitaka wakufuatilie kama wewe ni mlipaji wa kodi mahakama haiwezi kufanya chochote
Unaonekana ni kilaza kanisa halitozwi kodi wala zaka hazitozwi kodi ni ukilaza kufananisha kanisa na duka la mtaani
 
Unaonekana ni kilaza kanisa halitozwi kodi wala zaka hazitozwi kodi ni ukilaza kufananisha kanisa na duka la mtaani
Wewe ndio kilaza

Unaendeshwa kwa mhemuko badala ya kufikiri

Kwani ni kanisa inayopigiwa mahesabu au RAIA "kakobe"
 
mawakili mmekaa kutetea ujinga tu!! Hivi nyinyi hamna mawazo yoyote ya kumshauri rais Kuhusu maendeleo ya nchi yetu
Kwa,taarifa yako kila wakili atakayemgusa ni usalama wa taifa Kakobe ajiandae kuumia Ndani ya kanisa na nje ya kanisa ila kayataka Alivyoligema atalinywA shenzi type
 
Kwa,taarifa yako kila wakili atakayemgusa ni usalama wa taifa Kakobe ajiandae kuumia Ndani ya kanisa na nje ya kanisa ila kayataka Alivyoligema atalinywA shenzi type
Uzuri hao usalama wa taifa hawako upande mmoja tu wa bwana yule wa ukanda ule! Wanajua kuna maisha baada ya miaka 3 ijayo
 
Back
Top Bottom