Kesi ya askofu kakobe na TRA itakavyokuwa mahakamani.
WAKILI---- Shahidi wewe ni kamishna wa TRA?
SHAHIDI ---Ndiyo.
WAKILI---Ni kitu gani kilifanya muanze kufuatilia ulipaji kodi wa askofu kakobe?
SHAHIDI---Tulianza kufuatilia ulipaji kodi wa kakobe siku ile aliposema ana pesa kuliko serikali.
WAKILI---Ni kosa kusema kuwa una pesa kuliko serikali?
SHAHIDI---Hapana.
WAKILI---Je kuna sheria yoyote inayokataza mtu kumiliki pesa kuliko serikali?
SHAHIDI----Hapana
WAKILI----Ulishawahi kuwa mnafiki?
SHAHIDI ---Hapana
WAKILI---Ulishawahi kujipendekeza kwa wakubwa zako kazini?
SHAHIDI----kimyaa
WAKILI---Jibu mheshimiwa hakimu anakusubilia aandike jibu lako.
SHAHIDI---Sikumbuki,,
WAKILI-----Kakobe alipokuambia ana pesa kuliko serikali wewe ulijua serikali gani?
SHAHIDI---Serikali kuu ya nchi inayoongozwa na mtukufu rais?
WAKILI----Je katika maneno ya askofu kakobe kuna sehemu yoyote kuna maneno uliyoyataja wewe ya (SERIKALI YA MTUKUFU RAIS)
SHAHIDI---Hapana
WAKILI----Sasa kama kama hapana kwa nini wewe unataka kumuongezea maneno askofu kakobe?
SHAHIDI----Simuongezei ila nilikuwa nahisi alimaanisha serikali hii inayoongozwa na mtukufu.
WAKILI---Unakubaliana na mimi kuwa mahakama haiamini katika ushahidi wa kuhisi?
SHAHIDI---sijui
WAKILI ---Kakobe akija hapa na akaisibitishia mahakama kuwa yeye aliposema ana pesa kuliko serikali alimaanisha yeye ana pesa kuliko serikali ya mtaa au kijiji, je utakubaliana na mimi kuwa ulikurupuka kumshtaki kakobe?
SHAHIDI---Kimyaaa
WAKILI-----Unakubaliana na mimi kuwa maisha ya askofu kakobe yanaendeshwa na sadaka za waumini wake kwa kuwa kazi yake ya kila siku nikuwahudumia kiroho waumini wake?
SHAHIDI-----Ndiyo
WAKILI------Unafahamu askofu kakobe ana makanisa mangapi africa na america?
SHAHIDI-----Sijuii
WAKILI -----Unafahamu askofu kakobe ana waumini wangapi africa na america?
SHAHIDI-----Sijui
WAKILI-------Unafahamu kakobe anaingiza sadaka kiasi gani kutoka waumini wake hapa africa na america?
SHAHIDI-----Sijui
WAKILI-----Je kuna sheria yoyote iliyotungwa na bunge au chombo chochote chenye mamlaka inayotaka sadaka zikatwe kodi?
SHAHIDI-----Hakuna.
WAKILI------sasa ni kodi gani mnafuatilia kwa askofu kakobe kama sadaka hazitozwi kodi?wala hujui idadi ya waumini na sadaka anazopata kutoka kwa waumini wake?
SHAHIDI----Kimyaaaaa