LGE2024 Askofu Konki: Mtanzania usiuze kura yako kwa wagombea

LGE2024 Askofu Konki: Mtanzania usiuze kura yako kwa wagombea

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Viongozi wa Dini mkoani Manyara wametoa wito kwa vyama na wagombea wa vyama vya siasa kutumia lugha za kistaarabu wakati wa kampeni za uchaguzi wa Serikali za Mitaa zinazoanza Novemba 20 mwaka huu ili kudumisha amani, upendo na mshikamano wa kitaifa.

Soma, Pia: Yanayojiri kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Mkoa wa Manyara - Novemba 27, 2024


Askofu Mkuu wa Kanisa la Elim Pentekoste Tanzania Dkt. Peter Konki amewasisitiza wagombea kuepuka kuchafuana wenyewe kwa wenyewe huku akiwataka wananchi wasiuze kura zao kwa wagombea.

Kwa upande wake katibu wa Baraza kuu la waislamu BAKWATA wilaya ya Babati Abdi Ramadhani Isuja ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kusikiliza sera za wagombea kwenye mikutano ya hadhara ya kampeni ili wajue viongozi wa kuwapigia kura siku ya uchaguzi wa Serikali za mitaa Novemba 27 mwaka huu.
 
Back
Top Bottom