Askofu Munga ni Mlutheri lakini amezikwa na Waanglikani

Kwani alizaliwa na hao walutheri? Hata angezikwa na waumini wa dini za asili ambayo ndiyo asili yake. Hivi, haya yanatusaidia nini kama waathirika na watumwa wa hizi dini tapeli na uchwara yarabi?

..unaziita dini uchwara halafu umemaliza na neno "yarabi"?!
 
Maisha ni ubatili laiti angelifahamu hilo mwanzo naamini asingelikubali kusali KKKT
 
Huu mtindo upo sana tu. Kuna madhebu ukizinguana nao ukaja kufa hawakuziki, utazikwa kibudu kama hakutakuwa na dhehebu litakojitokeza kukuzika. Madhehebu mengine hujitokeza kuzika wafu waliaoachwa na madhehebu yao waliyokuwa wanaabudia huko kabla ya kuzinguana. Na kuna madhehebu hata kama ulizinguana nao watakuzika huku wakisema uovu wako
 
Kuna katekista aliponea chupuchupu kupigwa na waombolezaji baada ya kukataa kuendelea na ibada ya mazishi akidai marehemu alikuwa hahudhurii kanisani wala jumuiya haendi. Wazee wa busara walimpandisha bodaboda na kutoka nduki kukimbia hasira za waombolezaji
 
Hizi abrakadabra za kuzika kidini zipo hata kwa waislam. Kuna muislam mvuvi alifia majini wakaja kumfanyia taratibu za mazishi ya dini yao masheikh wakasema watamfinyia baadhi ya taratibu lakini zingine hawatafanya huko nyumbani kwake kwa kuwa marehemu alikuwa hahudhurii mikutano yao ya kidini.
 
Yaani wanamchamba marehemu...
 
Kwa waislam wakikuta mtu kafa hana ndugu wanaoleweka watajitahidi kujua jina lake kama ni mwislam wamzike kwa taratibu ya dini yao. Hawa wengine utazikwa kibudu bila hata pambio
 
Kuna jamaa mmoja alifariki kwa ajali ya pikipiki kwa kuanguka peke yake akiwa hana abiria. Aliacha kwenda kanisani miaka mingi, kanisa lake halikujishughulisha na msiba wake licha ya kuhudhuria msibani sawa na waombolezaji wengine. Nyimbo za maombolezo zikawa zinaimbwa kama kawaida zikiwemo nyimbo za maombolezo za chama chake cha siasa. Kwa kuwa huyo jamaa alikuwa na wadhifa wa kisiasa ngazi ya kata ikabidi chama chake kishike hatamu shughuli zote za msiba na mazishi, tena walikuja na sare zao za chama. Viongozi wa chama wa ngazi ya juu wakasoma neno na kuhubiria waombolezaji kama vafanyavyo wachungaji misibani. Jamaa alizikwa kichama, wenzake wasioenda makanisani huzikwa kibudu bila taratibu za kidini na madhehebu yao
 
Lakini wakristo ni wanafiki sana,wanafika msibani na misuti yao,ukiwaambia kuchimba kaburi wanagoma,haya tuingize mwili wa muumini kaburini (hawataki) wanarudi nyuma wakijifanya kuimba nyimbo. Hata kushika spedi kurushia udongo hawakuhusiki.
Misiba ya kikristo wanaozika ni vijana wa vijiweni
 
Kuna mchungaji najishauri kwenda kumpa ushauri awe anazika waumini wake walioacha kwenda kanisani badala ya kuacha muumini wake azikwe kibudu kama kufukia mzoga tu. Awe anatoa mahubiri kwa walio hai huko mazishini
 
kuna wale vijana wa Arusha, wachuga, wana matusi balaa misibani, wanakuambia hata wao wanaweza kusoma neno na wakamzika mwenzao, huwapa maneno makali viongozi wa dini kama endapo watachelewesha mambo. Wanafukia kaburi kwa mikono
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…