Dalton Elijah
JF-Expert Member
- Jul 19, 2022
- 968
- 1,978
PASCHAL MAYALA NA KABURI LA MEDIA!
Nimeona taarifa inayosema Baraza la Ithibati la Waandishi wa Habari limempa Paschal Mayala saa 24 athibitishe kauli yake kuwa Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba alichukizwa na kitendo cha waombolezaji wa msiba wa Kadinali Pengo kuwashangilia mawaziri wakuu wastaafu huku yeye hakushangiliwa.
Baraza la Ithibati limejiingiza katika mtego wa kitaaluma na kujichafua. Msiba ule wa Kadinali Pengo uligubikwa na hisia na majonzi na hivyo ulimgusa kila mtu.
Mimi niliposikia taarifa ya msiba huo, sikuweza hata kuandika chochote! Inawezekana ukimya wangu ulitafsiriwa kwa namna tofauti na watu wa makundi mbalimbali. Nilikuwa na haki pia ya kuonyesha hisia zangu kwa kukaa kimya na watu wengine walikuwa pia na haki ya kutafsiri huo ukimya wangu - ndio hisia zenyewe hizo!
Mawaziri wakuu wastaafu walipofika, walizua hisia ndani ya hisia. Watu wakawapigia makofi kuonyesha hisia zao. Huenda watu wakasahau kuwa msibani. Kila mmoja alikuwa na uhuru wa kutafsiri hisia zile. Huenda ikitafsiriwa ya kuwa pamoja na kuwa hawako katika madaraka yao, lakini bado wamekuja.
Lakini Waziri Mkuu alipoingia na itifaki yake, huenda shangwe zilipungua. Inawezekana pia shangwe zilipungua kwa sababu waombolezaji waliona kuwa yeye alikuja kutimiza wajibu kwa kuwa alikuwa madarakani. Huwezi kushangilia mtu anayetimiza wajibu wake. Lakini huenda pia shangwe zilipungua kwa sababu itifaki yake ilipoingia watu wakakumbuka tena kuwa wapo msibani - huenda itifaki aliwakumbusha hivyo wakaondoa shangawe wakaanza kumtafakari zaidi mwenzake Baba Kadinali.
Lakini watu waliokuwa nje wakitazama kwa luninga walikuwa huru kutafsiri hisia zile huku wengine wakifikiri kuwa shangwe ziliashiria pia kupendwa kwa wastaafu na ukimya uliashiriwa kununiwa kwa aliyepo! Wana haki ya kutafsiri hivyo kwa kuwa hisia ndiyo mali pekee ambayo mtu anaweza kumiliki peke yake.
Lakini Dkt. Mwigulu na yeye baada ya hapo pia alisikika akitoa hisia zake kuhusu tukio lile na tafsiri za watu.
Alisikika akisema 'hakuteuliwa' ili apendwe! Hizo nazo ni tafsiri zake kuhusu hisia za watu wengine. Na yeye piaalikuwa na uhuru wa kutafsiri hisia za watu wengine.
Paschal Mayala na yeye pia katoa hisia zake na hizo hisia kazitoa kwa njia ya kutafsiri hisia za Dkt. Mwigulu. Chuki au upendo na mali fikirika ambayo haiwezi kuthibitishwa mahakamani. Ni kwa sababu hizo mahakama nyingi duniani pia huogopa kutoa hukumu kuhusu vihisishi!
Sasa mtu anaposema nahisi fulani kachukua au kafurahi tangu lini hilo linaweza kuwa kosa? Baraza la Ithibati linapaswa kujikita na makosa ya kimaadili, sio hisia za watu. Hisia ni mambo ambayo hayapimiki na hivyo hayathibitiki! Je, ni kosa mtu kufikiri kuwa kiongozi amekasirishwa au amefurahishwa?
Katika taaluma ya sayansi ya uandishi wa jamii (sociology of media), Mayala hajatenda kosa lolote linalogusa maadili katika fani ya uandishi wa habari (media professionals etiquetes). Na hivyo tunafikiri kuwa Baraza la Ithibati bado liko katika uchanga.
Baraza linataka kuwafunga midomo waandishi wa habari wasiwe wanatoa hisia zao, wasiwe huru kujadili. Kama waandishi wa habari nchini wanajua haki zao, wanaweza kugoma kuandika na kuripoti au kutangaza habari zozote kuhusu viongozi wa serikali hadi Baraza liondoe kauli yake dhidi ya Paschal Mayala.
Vinginevyo kama waandishi wa habari pamoja na watangazaji watakaa kimya, kesho na wao watawekwa kitanzi kwa kuelezea hisia za Rais, Makamu wake au Waziri Mkuu. Mwandishi wa habari aliyekomaa ni yule anayekwenda mbali zaidi hata kwa kuelezea hisia za viongozi. Hiki ndicho alichokifanya Paschal Mayala. Lakini ni kama Baraza linataka kuzuia uandishi habari wa aina hii nchini! Twafwa!
Paschal Mayala akisalimu amri kwa amri hiyo isiyokuwa na nguvu ya kimaadili, atachangia pakubwa katika kuchimba kaburi la waandishi wa habari na watangazaji nchini Tanzania!
Je, nini kimekushangaza? Je, nini maoni yako?
Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Itunge, Dar es Salaam; 3 Februari 2026; Saa 2:15 usiku