Pre GE2025 Askofu Mwamakula aonya Uchaguzi wa ndani wa CHADEMA

Pre GE2025 Askofu Mwamakula aonya Uchaguzi wa ndani wa CHADEMA

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
Watu waliohujumu wenzao na kupora kura za Uchaguzi Mkuu wa 2020 hawana tofauti na watu wanaohujumu wenzao katika chaguzi zao ndani ya vyama. Kama Chadema watasahau machozi na maumivu ya kuhujumiwa Uchaguzi wa 2020, na kama pia watashindwa kusimamia haki katika chaguzi zao za ndani basi watakosa kabisa nguvu ya kimaadili ya kulaumu endapo watahujumiwa tena katika Uchaguzi wa 2025.

Manung'uko na tuhuma zinazosikika kuhusu kufinywa haki za wagombea katika baadhi ya maeneo katika chaguzi za ndani ya Chadema hayawezi kufumbiwa macho labda kama sote tutakumbatia unafiki. Lakini Chadema wanayo nafasi ya kipekee ya kushughulikia na kudhibiti upungufu huo, vinginevyo watapoteza imani iliyojengwa kwa muda mrefu na kwa gharama! Kama chama hicho kitashughulikia kwa haki na usawa na uwazi rufaa zote zilizokatwa na zile ambazo zitakazotwa kitajisafisha na kuimarika zaidi kuzidi vipindi vyote vya nyuma.
 
Watu waliohujumu wenzao na kupora kura za Uchaguzi Mkuu wa 2020 hawana tofauti na watu wanaohujumu wenzao katika chaguzi zao ndani ya vyama...
Huu ndio ukweli ambao makamanda wengi hawataki kuusikia, usafi unahitajika kufanyika ili kurejesha imani iliyokuwepo
 
Back
Top Bottom