BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,165
Mkristo unamwambia Askofu Mwamakula kuwa asichanganye dini na siasa?! Hujui kuwa kesi ya Yesu ilikuwa ni ya kisiasa? Hujui kuwa kesi ya Mtume Paulo ilikuwa ni ya kisiasa? Hivi haujui kabisa kuwa hata aliyeuzika mwili wa Yesu alikuwa ni Mwanasiasa? Hivi haujui kuwa Injili ya Luka na Kitabu cha Matendo ya Mitume vilielekezwa kwa mwanasiasa maarufu? Hivi hujui kuwa mmoja wa wanafunzi wa Yesu alikuwa ni mwanaharakati, mpigania uhuru na mwanasiasa?
Mkristo kweli unao ujasiri wa kumwambia Askofu Mwamakula kuwa asichanganye dini na siasa? Hujui kuwa muingiliano wa dini na siasa ndio uliopelekea uinjilishaji kufanyika kwa ufanisi wakati wa Mfalme Constantino aliyekuwa mtawala katika Dola ya Kirumi katika Karne ya Nne? Hivi hujui kuwa misukumo ya kisiasa ndio iliyopelekea kuzaliwa kwa Roman Catholic Church na Orthodox Catholic Church mwaka 1054? Hivi haujui kabisa kuwa misukumo ya kisiasa ilihusika pia katika kuanza kwa Kanisa la Moravian mwaka 1400?
Hivi Mkristo unafikiri kuwa theologia na mambo ya Liturgia tu ndio yaliyofanya Roman Catholic Church ligawanyike na kuzaliwa Lutheran kati ya mwaka 1517 na 1535? Hivi haujui kuwa Martin Luther alikuwa anatetea haki ya Wajerumani kujitawala? Hivi hujui kuwa Martin Luther alikuwa ni mpigania uhuru kule Ujerumani na ndio maana alikuwa analindwa na watawala wa Ujerumani? Hivi hujui kuwa Martin Luther kwa maneno mengine alikuwa anapigania Katiba Mpya kwa ajili ya Ujerumani?
Hivi Mkristo hujui kuwa Kanisa Anglikana lilianzishwa kwa sababu ya misukumo ya kisiasa? Hivi kweli hujui kuwa misukumo ya kisiasa, kijamii na mazingira duni ndivyo vilivyopelekea kuzaliwa kwa Assemblies of God Church kule Azusa, Marekani miaka 100 iliyopita?
Hivi hujui kuwa hata kuanza kwa Kanisa hapa Tanzania kulihusisha mahusiano kati ya dini na siasa? Hivi unafikiri unabii wa Amos, Isaya, Yeremia, Mika, Habakuki, Hosea na kadharika vilielekezwa kwa nani kama sio kwa viongozi wa kisiasa katika Karne zao?
Hivi haujui kuwa hata siri ya Mwalimu Nyerere kujua kuhusu hali ya koloni la Tanganyika ilitoka kwa Padre Welsh? Hivi unajua kuwa Mungu alihakikisha kuwa wana wa Israeli wanapata Katiba nzuri kabla ya kuingia nchi ya Kanani?
Ni maiti pekee ambaye hawezi kushiriki siasa kwa sababu haiwezi kula wala kuongea na pia haina hisia na wala haisikii maumivu na ndio maana mnaweza kuipeleka popote kwenda kuizika isibishe wala kukataa!
Ninatimiza wajibu wangu (Ezekieli 33:1-20)!
Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfutate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula no