Askofu Mwamakula; Je, nakosea na kuchanganya dini na siasa?

Acha kubabaisha watu. Mbona yesu aliwaambia wafuasi wake mpeni kaisari vilivyo vyake na mungu vilivyo vyake? Kwanza huyo mwamakula kanisa wanatakiwa wamtimue uaskofu maana anachofanya hajatumwa na kanisa lake wala sio sera ya kanisa askofu kua mwanasiasa wakati huohuo. Concempt ya kutenga mamlaka ya dini na serikali haikuanza leo na iko kikatiba kwa nchi nyingi. Akitaka avue dogcolar aanzishe au kuingia chama cha siasa.
 
Nataka nichukue hili andiko kama lilivyo nilisevu sehemu, ni ugali wangu tosha wa kifikra.

Kama hivi vichwa vichache vikiangamizwa hili taifa litabaki na kizazi cha wapumbavu ambacho kitaendelea kuzaliana kwa miaka mingi ijayo, hii elimu kutoka hawa maaskofu kama kuna asiyeipenda hakika ni wakala wa shetani.
 
Ndugu zangu watanzania suala la katiba ni lakila mmoja hata nyie CCM uwepo wa katiba nzuri utachochea mustakbali mwema kwa taifa
 
Ila wanasiasa hao na washabiki wao wakipewa nafasi madhabahuni wala hawaoni kuwa ni uchanganyaji wa dini na siasa!
Baba Askofu songa mbele!
 
Bravo Askofu. Wamewasahau michango ya ma-Askofu Desmund Tutu na Banana katika kupigania haki na uhuru wa SA na Zimbabwe. Endelea na mapambano baba. Usitizame nyuma ukageuka mnara wa chumvi. Tunakuunga mkono. You are not alone.
 
Kwa hiyo ukihukumiwa kisiasa kutokana na uchochezi wa kisiasa usilalame. Si ungeanzisha kabisa chana cha siasa ili upate mawanda mapana zaidi ya kupitishia maono yako???
Bado hujaelewa kabisa. Na sidhani kama utaelewa kwa upeo huo. Si lazima uanzishe chama ili uongelee na siasa. Anamaanisha popote penye uhai lazima pawe na siasa. Kuishi kwako vibaya au vizuri kinategemea siasa iliyopo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…