Askofu Mwamakula: Kampeni dhidi ya UKIMWI Mbeya ziepuke udhalilishaji

BAK

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2007
Posts
124,790
Reaction score
288,165
KAMPENI DHIDI YA UKIMWI MBEYA IEPUKE KUDHALILISHA UTU NA ISIKIUKE HAKI ZA BINADAMU!

Siku chache zilizopita tuliwasikia viongozi katika Mkoa wa Mbeya akiwemo Mkuu wa Mkoa huo wakiongea mbele ya kamera kuhusu Kampeni dhidi ya UKIMWI. Viongozi hao walisisitiza kuhusu adhma yao ya kuanzisha utaratibu wa kutumia shuruti ili kuwataka watakaobanika kuwa na virusi vya UKIMWI kuwataja watu wote walioshiriki nao mapenzi ili nao wapimwe [kwa shuruti]!

Kauli hizo za Viongozi katika Mkoa wa Mbeya zinaweza kuonekana kama ni njia na mkakati mzuri wa kupambana na UKIMWI. Lakini kauli hizo zikitazamwa kwa umakini, zinaweza kuwa na madhara makubwa sana. Utaratibu wo wote wa kutumia shuruti kutaka kumlazimisha muathirika wa UKIMWI kuwataja wapenzi wake wote ili nao wapimwe kwa shuruti utaleta madhara makubwa sana. Maana yake ni kwamba hao waliotajwa nao watashurutishwa kuwataja wengine na wengine na wengine!

Madhara ya utaratibu huo ni pamoja na Serikali kufedhehesha watu wake kwa nguvu, kuanza kuingilia kwa nguvu faragha za watu, kukiuka utu, na hata kukiuka haki za binadamu. Kibaya zaidi ni pamoja na kuleta au kuibua migogoro mikubwa ya ndoa kwa kuwa zoezi hilo halitaweza kufanyika bila watu wengine kujua na hata wana ndoa.

Mkoa wa Mbeya ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo imeingia na kuridhia mikataba mingi katika Jumuiya ya Kimataifa ikiwemo mikataba ya kiutu na ile ya Haki za Binadamu. Hivyo, viongozi wote katika ngazi zote wajitahidi kuheshimu utu na Haki za Binadamu katika sehemu zao za kazi.

Kwa tabia hizi za viongozi kutoa matamko, maelekezo, na amri zinazoathiri maisha ya watu nje ya mifumo ya kisheria, tusipozikemea tabia hizo tutakuwa tunaondoa taratibu mifumo ya uongozi wa kidemokrasia na badala yake tutajikuta tunatawaliwa na madikiteta katika ngazi zote kuanzia vitongoji, vijiji, kata, tarafa, wilaya, mkoa na hata katika Serikali Kuu!

Mimi kama Askofu nauona mpango wanaotaka kuutekeleza viongozi wa Mkoa wa Mbeya unaweza kuleta madhara makubwa kwa jamii. Kuna hatari athari hizo zisiishie Mbeya tu bali zikavuka mipaka ya Mbeya kutokana na mwingiliano wa watu kwa njia ya makazi, biashara na kuoana! Ninashauri taasisi na makundi ya kutetea utu na Haki za Binadamu katika nchi hii waliangazie kwa umakini jambo hilo ili kujiridhisha kama halitadhalilisha utu na wala halitakiuka Haki za Binadamu!

Miko nimekwisha kutimiza wajibu wangu (Ezekieli 33:1-20).

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!

Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula - Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki
 
Hata mm nashangaa,, namlinganisha kama yule aliyeshindwa kuapa
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Huyu askofu sasa hivi kawa mwandishi wa habari?
 
Mgonjwa ana haki zake, linalomsibu ni lake na tabibu wake. Wanasiasa wataka sifa kwa aliyewateua wasiingilie taalu.s za watu. Bila shaka waziri wa afya atatoa tamko.
 
Ningekuwa Mbeya,halafu nikawa kwenye list na kulazimishwa kuwataja niliowagegeda ningemtaja Bi Calm
 
Siasa na wokovu wapi na wapi?
KAMPENI DHIDI YA UKIMWI MBEYA IEPUKE KUDHALILISHA UTU NA ISIKIUKE HAKI ZA BINADAMU!

Siku chache zilizopita tuliwasikia viongozi katika Mkoa wa Mbeya akiwemo Mkuu wa Mkoa huo wakiongea mbele ya kamera kuhusu Kampeni dhidi ya UKIMWI. Viongozi hao walisisitiza kuhusu adhma yao ya kuanzisha utaratibu wa kutumia shuruti ili kuwataka watakaobanika kuwa na virusi vya UKIMWI kuwataja watu wote walioshiriki nao mapenzi ili nao wapimwe [kwa shuruti]!

Kauli hizo za Viongozi katika Mkoa wa Mbeya zinaweza kuonekana kama ni njia na mkakati mzuri wa kupambana na UKIMWI. Lakini kauli hizo zikitazamwa kwa umakini, zinaweza kuwa na madhara makubwa sana. Utaratibu wo wote wa kutumia shuruti kutaka kumlazimisha muathirika wa UKIMWI kuwataja wapenzi wake wote ili nao wapimwe kwa shuruti utaleta madhara makubwa sana. Maana yake ni kwamba hao waliotajwa nao watashurutishwa kuwataja wengine na wengine na wengine!

Madhara ya utaratibu huo ni pamoja na Serikali kufedhehesha watu wake kwa nguvu, kuanza kuingilia kwa nguvu faragha za watu, kukiuka utu, na hata kukiuka haki za binadamu. Kibaya zaidi ni pamoja na kuleta au kuibua migogoro mikubwa ya ndoa kwa kuwa zoezi hilo halitaweza kufanyika bila watu wengine kujua na hata wana ndoa.

Mkoa wa Mbeya ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo imeingia na kuridhia mikataba mingi katika Jumuiya ya Kimataifa ikiwemo mikataba ya kiutu na ile ya Haki za Binadamu. Hivyo, viongozi wote katika ngazi zote wajitahidi kuheshimu utu na Haki za Binadamu katika sehemu zao za kazi.

Kwa tabia hizi za viongozi kutoa matamko, maelekezo, na amri zinazoathiri maisha ya watu nje ya mifumo ya kisheria, tusipozikemea tabia hizo tutakuwa tunaondoa taratibu mifumo ya uongozi wa kidemokrasia na badala yake tutajikuta tunatawaliwa na madikiteta katika ngazi zote kuanzia vitongoji, vijiji, kata, tarafa, wilaya, mkoa na hata katika Serikali Kuu!

Mimi kama Askofu nauona mpango wanaotaka kuutekeleza viongozi wa Mkoa wa Mbeya unaweza kuleta madhara makubwa kwa jamii. Kuna hatari athari hizo zisiishie Mbeya tu bali zikavuka mipaka ya Mbeya kutokana na mwingiliano wa watu kwa njia ya makazi, biashara na kuoana! Ninashauri taasisi na makundi ya kutetea utu na Haki za Binadamu katika nchi hii waliangazie kwa umakini jambo hilo ili kujiridhisha kama halitadhalilisha utu na wala halitakiuka Haki za Binadamu!

Miko nimekwisha kutimiza wajibu wangu (Ezekieli 33:1-20).

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!

Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula - Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki
 
Je kampeni imetekelezwa?
Je umehama kwenye hoja ya maandamano?
Je unamchokoza mkuu wa mkoa ili u test vyombo?
Hivi lini huwa unakaa madhabahuni na kufanya kazi ya uaskofu?
 
Back
Top Bottom