Mtanzania2020
JF-Expert Member
- May 23, 2020
- 817
- 1,752
MATOKEO YA MKATABA WA MILELE KATI YA ESSAU NA YAKOBO KWA VIZAZI VYAO VYOTE!
Madhara ya mkataba kati ya Essau na Yakobo yalikuja kuonekana baadaye baada ya Essau kupoteza kabisa haki zake zote za kiutawala, kiuongozi, kiuchumi, kidiplomasia na kisiasa. Chanzo cha mkataba ule ilikuwa ni tamaa ya Essau ya kupata pesa ya kufanyia shopping, kula nyama choma na kunywa supu ya pweza.
Baada ya Yakobo kugundua kuwa Essau alitaka sana apate hela ya matanuzi na supu ya pweza, aliweka sharti la kuandikiana mkataba. Lakini kwa kuwa akili ya Essau ilikuwa katika kupata vile vitu na jinsi atakavyowalingishia wenzake wa Mesopotamia, hakuweza hata kuwa makini kuangalia vipengere vya mkataba na wala yeye hakuona shida mkataba kuandikwa na Yakobo.
Baadaye alipokuja kushtuka akakuta mkataba ulikuwa hauna ukomo - ulikuwa ni wa milele na kuwa Yakobo alikuwa amejimilikisha kila kitu. Lakini Essau alipotaka kubadili vile vipengere vibaya ndani ya mkataba, Yakobo alikataa lakini hata Mahakama ya rufani chini ya Mzee Isaka ilisema kuwa mkataba ule hauvunjiki. Mkataba ule ulipora haki zote hata za vizazi vya Essau katika nyanja zote - kidiplomasia, kiuchumi, kiutawala, kisiasa, nk (Mwanzo 25).
Wataalamu wengi wa Biblia wanakubaliana pia kuwa uzao wa Yakobo ndilo taifa la Israeli na uzao wa Essau ndilo taifa la Jordan. Je, kama hiyo ni kweli kuhusu historia ya mataifa hayo mawili yaliyo jirani, unayaonaje mahusiano ya nchi hizo mbili na hasa ushawishi wa kila nchi katika jumuiya ya kimataifa kisiasa, kiuchumi, kijeshi na kidiplomasia?
Uliwahi kusoma kisa cha Essau na Yakobo kwa jicho la mkataba? Unafahamu kuwa mikataba yote inayohusu rasilimali inahitaji umakini sana kwa kuwa mtu akikabidhiwa rasilimali haziachii kirahisi? Unafikiri ni kwa nini Yakobo aliandika mkataba mwenyewe bila kumshikirisha Essau?
Je, nini kimekushangaza? Je, nini maoni yako?
Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki
Dar es Salaam, 22 Julai 2023; 07:08 am