Askofu Mwamakula na matembezi ya hiyari Nchi nzima

Kule kwa Trump walioandamana anashikwa mmoja mmoja kama anataka kuandamana amtangulize kwanza anayemshauri kiroho arudi kutoka Ubelgiji na pia yule aliyekimbilia Kanada nae arudi kwanza waongoze hayo matembezi,kama anataka matembezi ya hiari si kila siku anayafanya ,kama anataka matembezi ya hiari awaamurishe kondoo wake .Mwamakula kageuka kituko kakanisa kake kanamshinda halafu leo anataka awaamurishe Watanzania,anaye msikiliza Mwamakula ana matatizo.
 
Anajitahidi kuonyesha stress zake hadharani....

Lakini ana hoja nzito.

Soon or later...
 
Hii inayoratibiwa na kiongozi wa dini haiwezi kufanikiwa kwa sababu lazima itanasibishwa na dini yake. Italeta utengano zaidi. Ni vikundi secular tu ndivyo vinafaa kuhamasisha jambo kama hili
 
Hivi hata baba askofu naye hakujitokeza kwenye yale maandamano ya lisu? Naona kila kamanda anapambana kivyake kujitafutia promo!
 
Askofu hajaeleza nani atapokea matembezi hayo kila wilaya au mkoa. Huwezi kutembea tu hata treni ina kituo.
 
Hapa kwenye aya hii nimekuelewa vizuri Sana baba askofu Mwamakula
 
Ni imani yangu kuwa Mungu atasema na nafsi ya Rais na kwamba Mungu atanilinda sawasawa na Neno lake (Zaburi 121). Lakini hata hivyo, hata kama Mungu katika hekima yake isiyoweza kuhojiwa ataruhusu mabaya yanaipate sitaweza kuogopa na nitaongoza Matembezi ya Hiyari kwa kuwa dhamiri yangu mbele za Mungu hailaumiki kuhusiana na jambo hili (Isaya 6:8-13).
 
Trump alitaka kupora uchaguzi Marekani akapigwa chini huyo anayejiita mwendawazimu kapora uchaguzi hapa. Sasa uhusiano wa matembezi ya kudai katiba mpya na tume huru na Trump kutaka kupora uchaguzi uko wapi? [emoji15]
Hajitambui huyo achana naye
 
Huyu Askofu asituchanganye.
Sie tupo busy na "maandamano yasiyo na kikomo" ya Tundu Lisu
 
Askofu mwenzake Bagonza na Kigogo wanasema kuna Corona.leo Huyu anataka kuua watu kwa kuwatembea watu Kwenye nchi ya Corona.police msipe kibari huyu aliyejivalisha uaskofo wakati tunajua ni chadema na katumwa na chadema.mlikataa kupeleka wabunge bungeni leo mnataka Tume huru ya kufanya uchaguzi gani? Siasa peleka bungeni.na kanisa analoongoza lifungwe .
 
Asante Baba Askofu. Tupo pamoja.
 
Hata kama unalishwa na Lumumba, tumia akili. Si kwa ujinga huu!
 
Hapa inaonekana askofu anakiamini anachokizungumza, mtihani upo katika kudumisha kile anachokiamini, na hicho anachokiamini kuhimili utamaduni mgumu. Maana lipo Giza libebalo nuru, na ipo nuru ibebayo giza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…