Askofu Mwamakula: Rais Samia amegusa kila kitu bila kukisumbua

Askofu Mwamakula: Rais Samia amegusa kila kitu bila kukisumbua

BAK

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2007
Posts
124,790
Reaction score
288,165
AMEGUSA KILA KITU BILA KUKISUMBUA..

Hotuba imeisha. Tumeisikia. Penye wengi kuna mengi. Nimetoka na haya:

1. Hotuba nzuri lakini ya kawaida. Wakuu wa nchi wa kawaida huongea kwa uungwana mbele ya mabunge. Yaliyo mengi tumeyashika tangu utoto. Yalienda likizo awamu ya tano.

2. Kawa jasiri kugusa demokrasia na Haki za Binadamu. Vigelegele vilipungua. Sababu ipo. Awamu iliyopita haikuwa rafiki wa demokrasia na Haki za Binadamu. Wapiga vigelegele wasingeweza kunyea mbeleko. Nampongeza hata kwa kusema. Kutenda tunasubiri.

3. Mgongano upo. Mama na yeye kitu kimoja. Mmoja adui wa demokrasia na Haki za Binadamu, mwingine rafiki. Any way, Roma haikujengwa siku moja. Tungoje hata kama matumbo yanauma.

4. Kavitaka vyombo vya haki vitoe haki kwa mujibu wa sheria. Awamu iliyopita zilipitishwa sheria nyingi mbaya na kwa haraka. Haki ipi mbele ya sheria mbaya? Sheria mbaya huzaa haki mbaya.

5. Kaahidi kukutana na vyama vya siasa. Bila shaka alimaanisha vya upinzani kwa sababu cha kwake si cha siasa ni cha dola. Ahadi inasubiriwa. Ahadi imekosa vigelegele. Walipita bila kupingwa na demokrasia ikafa bila kupingwa.

6. Mwisho wa mwezi, Mama anakalia kiti cha chama dola chetu. Baada ya hapo akutane na vyama vya siasa. Akiwa nao atasahau kuwa yeye ni Mwenyekiti wa chama dola? Mashaka ni makubwa kuliko matumaini. Nia anayo, moyo wake u radhi, lakini mwili ni dhaifu. Hata hivyo anaonekana kuwa na ngozi ngumu. Kasema ruksa kukosoa. Tumuombee.

7. Hotuba imegusa vitu vingi. Mama ahsante. Kuna vitu nimevikosa na ni haki nivikose kwa sababu hotuba sikuandaa mimi. Nilitamani:

- Katiba mpya aliyoiongoza

- Maridhiano na wahanga wa awamu
Iliyopita

- Matamko yaliyokiuka katiba na
yanaendelea kutekelezwa

- Uhuru wa vyombo vya habari.

Nina mengine, nitamtafuta mama.
Namuombea mama. Ameshikilia mustakabali wetu. Kudemka kwa bunge hakujaisha.

Kazi Iendelee
 
Hivi kumbe kweli vigelegele vilipungua alivyogusia demokrasia?! lile bunge ni fake.

Na kuhusu kukutana na vyama vya upinzani huku tayari akiwa ameshapewa uwenyekiti wa chama chake hili, linaweza kuwa tatizo kama atakubali kusikiliza ushauri atakaopewa na chama chake.
 
Mambi ni mengi. Huwezi kufanya kila kitu ndani ya mwezi. Mpeni muda
 
Hivi kumbe kweli vigelegele vilipungua alivyogusia demokrasia?! lile bunge ni fake.

Na kuhusu kukutana na vyama vya upinzani huku tayari akiwa ameshapewa uwenyekiti wa chama chake hili, linaweza kuwa tatizo kama atakubali kusikiliza ushauri atakaopewa na chama chake.
Duh nyie watu akili zenu mnazijua mwenyewe. Siku zote Rais huwa na atakuwa ni mwenyekiti wa chama. Si unataka kuniambia wakati Kikwete anakutana na wapinzani hakuwa mwenyekiti wa chama. Wakati chadema iko kwenye peak, wakati wa Kikwete rais hakuwa mwenyekiti wa chama. Mbona mna tafuta hoja za kuokoteza. Kama hamuwezi kumpa tano bora mkae kimya
 
Askofu tumia mawazo yako kuimarisha kanisa lako na unawaongoza wanatosha sio lazima nyote mfanane hata huyo mkeo nyumbani sidhani kama anapendezwa na kila unachofanya!
 
Hapo kwenye 2 na 5 Askofu kaua; ghafla wademkaji wakawa kama wamemwagiwa maji kimya kikatawala.
 
Askofu tumia mawazo yako kuimarisha kanisa lako na unawaongoza wanatosha sio lazima nyote mfanane hata huyo mkeo nyumbani sidhani kama anapendezwa na kila unachofanya!
Kwa hoja zako humu sioni unacho mlaumu Askofi ni nini.
 
Back
Top Bottom