BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,165
VIONGOZI WA DINI WATUMIA TBC KUTOA MAONI YAO KUMSIFIA RAIS MAGUFULI.
Tarehe 9 Desemba 2020 majira ya Saa 9 asubuhi. Nipo katika runinga nikitazama na kuangalia kipindi maalum katika TBC. Kuna viongozi wawili wa dini, Askofu Sylivester Gamanywa wa WAPO Mission International na Sheikh Swed Twaib wa BAKWATA wanatoa maoni yao kuhusu Utendaji wa Rais Magufuli hususan Uteuzi wa Baraza la Mawaziri uliofanywa hivi karibuni. Wamesifia weredi, na umakini wa Rais katika kuunda Baraza lake la Mawaziri na kwamba amefuata viwango, vigezo na Katiba.
Hayo ni maoni ya viongozi hao wa dini. Wao wameamua kusifia na hicho walichokiona. Hatuwezi kusema wanafanya siasa au wanachanganya dini na siasa. Ni haki yao kikatiba lakini pia ni haki ya wananchi kusikia maoni ya viongozi wa dini wanaosifia utendaji wa Serikali.
Vilevile, ni vizuri tukaelewa kuwa wapo viongozi wa dini wanaotoa maoni yao kwa njia ya kukosoa, kuonya au kukemea pale wanapoona kuwa hapaendi sawa. Nao ni mtazamo wao na hatuwezi kusema kuwa wanafanya siasa au wanachanganya dini na siasa. Ni haki yao kikatiba na ni haki ya wananchi kusikia maoni ya viongozi wa dini wanaokuwa na maoni tofauti kwa kukosoa, kuonya na kukemea mambo yasiyokwenda sawa!
Tanzania tuwe tayari kusikia maoni ya viongozi wa dini yawe ya kusifia, kuonya, kukemea au kukosoa. Tunawatia moyo kuanzia Januari 2021 kujitokeza kwa wingi kusikiliza maoni ya Askofu Mwamakula kupitia "Matembezi ya Hiyari" kuhusu umuhimu wa Kuunda Tume Huru ya Uchaguzi na Uandikwaji wa Katiba Mpya!
Mwana Kondooo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula - Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki