Askofu Mwamakula: Viongozi waliojenga maadui, watatumia nafasi zao kudhibiti wengine

Askofu Mwamakula: Viongozi waliojenga maadui, watatumia nafasi zao kudhibiti wengine

BAK

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2007
Posts
124,790
Reaction score
288,165
MOYO WA ASKOFU MWAMAKULA KWA TAIFA

Unatafuta kuongoza Kitongoji, Kijiji, Kata, Jimbo, Wilaya, Mkoa na hata Taifa. Lakini unapanda miiba njiani ili kuwazuia washindani wako. Unatafuta uteuzi au hata ushindani wa kibiashara au unatafuta kushinda tenda Serikalini, lakini unatega mabomu ili kutaka kuwalipua washindani wako! Unataka nafasi ya kisiasa katika Chama chako, lakini unatembea na ndoo ya maji taka ili kummwagia mtu ye yote utakayekutana naye njiani. Unataka anuke ili asichaguliwe!

Ukishindwa kufanikisha hayo yote, miiba yako ikioza, mabomu yako yakishindwa kulipuka, maji taka yasipowapata walengwa; unabuni mbinu nyingine! Unaharibu biashara za washindani wako au hata unahakikisha wamefukuzwa kazi! Unamrushia jini mshindani wako. Likimkosa, unamuandalia sumu, ili aangamie kabisa. Vyote hivyo vikishindikana, unatafuta watu wasiojulikana unawalipa pesa ili wammalize kwa risasi!

Unafanya yote haya ili upande juu, ili upate uongozi, ili ushinde ushindani wa kibiashara! Ukifanikiwa katika adhma yako, unasahau kurudi nyuma kuja kuondoa miiba uliyoipanda njiani na unasahau hata kuja kutegua mabomu uliyotega. Hata kukumbuka kuja kuwanunulia sabuni wale uliowamwagia maji taka ili angalau waoge unashindwa! Si ukimbuke basi hata kuwatunza wale yatima, wajane na wagane wa wale uliowaua?

Jamii ikiwa na viongozi wa namna hii haiwezi kupata ustawi. Viongozi ambao wamejenga maadui kila mahali walikopita watatumia nafasi zao ili kujilinda na kudhibiti wengine. Uadui, chuki na visasi hutawala katika jamii. Kila kiongozi anapokuja atafichua uovu wa aliyetangulia kwa kuwa aliyetangulia alijikita zaidi katika kudhibiti wengine na kujilinda yeye.

Askofu Mwamakula ni ishara kwenu katika zamani hizi! Huu ujumbe unawahusu wengi usije ukafikiri unakwenda kwa Mayasa au Ndunguru! Ingawa ujumbe huu unawagusa sana wanasiasa, wafanyakazi na wafanyabiashara; viongozi wa Dini hawawezi kujitenga nao! Kwa sababu nao kwao yamesikika hayo hasa wale ambao nafasi za uongozi wa juu hupatikana kwa njia ya Uchaguzi.

Msihangaike na maumbile ya Askofu Mwamakula! Hangaikeni na ujumbe anaouwasilisha kwenu! Na ninyi CCM, ambao keshokutwa mna vikao nyeti! Dondosheni hizo ndoo zenu za maji taka! Mnabeba miiba ya nini enyi Vijana wa BAVICHA wakati wa kumtafuta Katibu Mkuu? Wanawake wanajulikana kwa huruma na ni walezi wazuri, hivyo hatutegemei watu wa BAWACHA kubeba mabomu wakati mnakwenda kumtafuta kiongozi wenu!

Naitamani siku ambapo nchi hii itatabasamu! Siku ambapo washauri wa Rais Samia watamtia moyo Mheshimiwa Rais kuwaongoza viongozi wa vyama vyote vya siasa nchini katika kuzika tofauti za kisiasa kwa njia ya maridhiano! Siku ambayo milango ya Magereza itakapotema mahabusu wote waliopelekwa kule kama njia ya kuwakomoa na kuwadhibiti! Machozi yanalowesha karatasi yangu! Nalazimika kunyamala! Nanyamaza! Ngubatama! Ngibile (Ezekieli 33:1-20).

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula - Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki
 
Asante baba askofu mwamakula, ki ukweli yule mwendazake alikuwa katili kuliko shetani. Mimi ni mhanga ni kati ya watu wachache niliopewa kesi ya rushwa kisa tu Niko upande wa pili. Licha ya kushinda kesi lakini bado nilitekwa na kuamuliwa kwa nguvu kupewa kadi ya kijani.

Yaliyofanyika kwa mwendazake yanatisha. Nitaelezea zaidi yaluyonipata tarehe 13.04.2020 ni zaidi ya unyama.
 
Asante baba askofu mwamakula, ki ukweli yule mwendazake alikuwa katili kuliko shetani. Mimi ni mhanga ni kati ya watu wachache niliopewa kesi ya rushwa kisa tu Niko upande wa pili. Licha ya kushinda kesi lakini bado nilitekwa na kuamuliwa kwa nguvu kupewa kadi ya kijani. Yaliyofanyika kwa mwendazake yanatisha. Nitaelezea zaidi yaluyonipata tarehe 13.04.2020 ni zaidi ya unyama.
Pole mkuu
 
Maisha ndio yalivyo, ndio maana kuna misemo kama vile "Survival for the fittest" Hata yeye Mwamakula kufikia hapo amepambania aonekane yeye na si wenzake. Maisha ndivyo yalivyo.
 
Hakika ujumbe umegonga moyo wangu Mungu atujalie uzima tuyaone hayo maono yako. Amen
 
Ahsante kwa ujumbe baba Askofu, Taifa lishaanza kutabasamu tangu March, muda unavoenda nadhani litacheka kabisa.
Amen.
Ujumbe ni mzuri sana. Tulikuwa na tatuzo la mapambio ya sifa sasa tatizo ni miluzi kumtisha au kumwambia nini afanye au asifanye. Inatakiwa kujivika Umandela, kusamehe na kupatanisha, kuponya vidonda bila kujali miluzi. Hiyo ndiyo itakuwa legacy kwa vizazi hata vizazi.

Miluzi haipaswi kumtisha na kuicha njia ili kuwaridhisha wapiga miluzi. Eti mimi na yeye ni mapacha. Noooo! Nafasi hii imetolewa na Mungu kipekee kuponya waja wake! Haijalishi, Musa aliitimia fimbo aliyopewa na Mungu dhidi wa watu wa firauni.
 
Ujumbe ni mzuri sana. Tulikuwa na tatuzo la mapambio ya sifa sasa tatizo ni miluzi kumtisha au kumwambia nini afanye au asifanye. Inatakiwa kujivika Umandela, kusamehe na kupatanisha, kuponya vidonda bila kujali miluzi. Hiyo ndiyo itakuwa legacy kwa vizazi hata vizazi.
Miluzi haipaswi kumtisha na kuicha njia ili kuwaridhisha wapiga miluzi. Eti mimi na yeye ni mapacha. Noooo! Nafasi hii imetolewa na Mungu kipekee kuponya waja wake! Haijalishi, Musa aliitimia fimbo aliyopewa na Mungu dhidi wa watu wa firauni
Sure
 
Shikamoo baba Askofu Mwamakula. Nakuamkia kwa jina la Tanganyika.
"Nyamala kulia baba Askofi"

Mwenyezi Mungu atakulipa pakubwa sana.. Duniani na ahera utakua na heri za Allah.. 🙏🏽🙏🏽🙏🏽
 
Mungu aendelee kumlinda na kumbariki balozi wake huyu mwema kwa Taifa letu. Kanisa lilipokosa mzungumzaji kwa ajili ya kumfueahisha Nduli mwendazake, ni Askofu Mwamakula peke yake hakuogopa jela wala mahakama, aliendelea kuongea ukweli na akihubiri haki.
 
Back
Top Bottom