The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 896
- 1,427
Askofu Mkuu wa Kanisa la Moravian la Uamsho, Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula ametoa wito kwa wale wanaomshikilia baada ya kumteka kijana Method Damian Kumdyanko na kuacha kuitisha familia na jamaa zake wa karibu.
Akizungumza kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yanayofanywa na Baraza la Wanawake CHADEMA leo jijini Dar Es Salaam Askofu Mwamakula ametoa wito kwa baraza hilo pamoja na CHADEMA kuendelea kuwa sauti ya kupigania mabadiliko katika taifa kwani itasaidia kupaza sauti za wale wasioweza kuongea au wasio na pa kusemea.
Soma pia: Pre GE2025 Dar: Method Damian Kumdyanko adaiwa kutekwa na watu wasiojulikana wakiwa na silaha
“Kama nyinyi CHADEMA mtajisemea ninyi hamtawasemea wanaotekwa haki yenu itatafsiriwa kama ni ubinafsi mtu yeyote anayefanyiwa visivyo anastahili kusemewa na ninyi” amesema Askofu Mwamakula
“nitumie nafasi hii kuwaambia wanaomshikilia kijana Method Damian Kumdyanko wamuachilie yule kijana siyo mwanaChadema taarifa zangu ni kwamba ameajiriwa na serikali” ameongeza Askofu Mwamakula
Method alitekwa Februari 28, nyumbani kwake Sinza Dar Es Salaam majira ya saa mbili usiku alipokuwa akiingia nyumbani.