Askofu Mwamasika ajitosa kuwania ubunge

ishuguy

Member
Joined
Nov 3, 2007
Posts
76
Reaction score
10
5th December 2009

Baada ya Mbuge wa sasa wa Jimbo la Dodoma Mjini kupitia (CCM), Ephraim Madeje, kutangaza kuwa hatagombea tena ubunge katika Uchaguzi Mkuu wa mwakani, Askofu mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Peter Mwamasika, ametangaza nia yake ya kugombea kiti hicho.

Dk. Mwamasika, alisema jana kuwa alikuwa anatafuta jimbo ambalo angeweza kugombea nafasi ya ubunge na kwa kuwa Mbunge wa Dodoma Mjini ametangaza kutokugombea ni wazi sasa ana haki ya kuchukua nafasi hiyo.

Alieleza kuwa pamoja na kuwa ni mstaafu katika nafasi ya uaskofu lakini bado ana uwezo wa kuwa mwanasiasa kwani hata kabla ya kushika nafasi ya uaskofu, alishawahi kuwa mbunge kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) katika Jimbo la Iringa Vijijini.

Askofu Mwamasika alisema kuwa ana kila sasabu ya kugombea Jimbo la Dodoma Mjini kutokana na wabunge wengi ambao wametangulia kutoleta maendeleo ya kweli katika jimbo hilo wakati lina rasilimali nyingi ambazo kama zikitumiwa vizuri, zinaweza kuwaondolea wananchi umasikini unaowakabili.

Aliongeza kuwa pamoja na serikali kuanzisha mkakati wa Kilimo Kwanza, lakini mkakati huo unaonekana kuwa itakuwa vigumu kuutekeleza kwani wananchi bado hawajaweza kupatiwa elimu ya kilimo na kupewa pembejeo za kutosha.

Askofu huyo mstaafu alisema kuwa inashangaza kuona wakazi wengi wa Dodoma wanaendelea kuwa ombaomba wakati wana utajiri mkubwa ambao unaweza kuwafanya kuishi maisha mazuri lakini kila mbunge ambaye ameshika nafasi hiyo amekuwa akijisahau na kuingia bungeni kama sehemu ya kujipatia maslahi yake binafsi.

Askofu Mwamasika alifafanua kuwa ili wakazi wa Dodoma waweze kuishi maisha mazuri na wakubaliane na sera ya serikali ni lazima wawezeshwe katika kufufua kilimo cha zabibu na wapatiwe soko la uhakikika la zao hilo.
Aidha, alisema kuwa Mkoa wa Dodoma una fursa nyingi na kiongozi ambaye anaongoza mji wa Dodoma anatakiwa kuwa mbunifu na mwenye uwezo wa kutafuta wafadhili ambao wanaweza kupeleka maendeleo katika jimbo hilo.

Alisema katika uongozi wake wa miaka 20 ambayo ameitumikia Dayosisi ya Dodoma, ameweza kubadilisha maisha ya waumini wa kanisa hilo na sasa hakuna muumini ambaye hana maendeleo.

Alibainisha kuwa kutokana na jitihada zake za kutafuta maendeleo ya watu wake, alifanya juhudi ya kujenga hospitali yenye hadhi ya rufaa na kuanzisha kiwanda cha maji ya A-Sante ambayo yanapatikana katika kijiji cha Ntyuka na kwamba wafanyakazi wa kiwanda hicho ni wenyeji wa kijiji hicho.

Alisema kuwa mgombea wa nafasi ya ubunge anatakiwa kujitambua na kuelewa kuwa ni mtumishi wa watu badala ya kuwa mtawala na kuhakikisha anatetea maslahi ya wananchi.

“Ni lazima kusimama kidete kuhakikisha nchi inafanikisha kuwawajibisha wale wote ambao wanaitwa mafisadi ambao mimi huwa nawaita wahujumu uchumi,” alisema Askofu Mwamasika, ambaye mara nyingi hukemea maovu katika jamii.

Hata hivyo, alisema CCM inatakiwa kuonyesha ujasiri katika kuwawajibisha wale wote wenye tuhuma za kweli za vitendo vya ufisadi ili wananchi waweze kuwa na imani na serikali iliyoko madarakani.


CHANZO:
NIPASHE:

Mheshimiwa Askofu anamalengo mazuri na inaonekana amejitahidi kufanya maendeleo kipindi cha uaskofu wake...
swali la msingi mbona hajazunguzia alifanya nini alipokuwa mbunge wa Iringa Mjini maana ndo post inafanana na anayoitaka sasahivi...
Asije akapata ubunge akapoteza malengo yake akatumbukia kwenye ufisadi..

kila la heri askofu
 
kila mtu ana uhuru wa kuingia kwenye politics but we need action sio promise za maisha bora kila siku
 
kazi kwake ila akumbuke dini inakataza rushwa sasa sijui hili atakabiliana nalo vipi! ila sikuhizi kuna kiongozi wa dini?si basi tu, ila hata mama wa misukule si yupo ndani ya nyumba hivyo atampa support
 
Hapa Askofu amechemsha,cheo cha Uaskofu kimaadili hakimruhusu kuingia katika siasa za majukwaani.
 
Yale yale. Ataweza kudeal na all the immorality and hooliganism huko bungeni hata akishinda? Mama Rwakatare kafanya nini hadi sasa?
 
Hii ndio picha halisi ya wengi Tanzania. Kwavyovyote vile target yake ni kupitia CCM. Ndio picha halisi inapatikana. Maana viongozi wa dini wanapiga kelele kumbe mifukoni mwao wanakadi za vyama vingine. Viongozi wa dini wanaongoza waumini wa vyama mbalimbali vya siasa. Sasa km kiongozi ni muumini wa chama fulani, sijui anaweza kuwa objective kwa mwanachama mwingine? Katika hali kama hii kauli kama huyu ametumwa na MUNGU mchagueni zitakuwa na mantiki? Sasa ndiyo tunaona hali halisi ya watumishi wa Mungu.
 
Hapa Askofu amechemsha,cheo cha Uaskofu kimaadili hakimruhusu kuingia katika siasa za majukwaani.

Nakuunga mkono mkuu....

Ila tusisahau huyu askofu amekuwa na mambo mengi ya kidunia kwa muda mrefu na hata kuna wakati wa ile vurugu ya ELCT alikuwa mmoja wao wale walioweka focus ya mkate kuliko neno!!!

Haya yote ni ishara tu ya baadhi ya watu kutoelewa na kuthamini hadhi ya madaraja waliyopewa kusadia watu kuishi maisha aliyoagiza allah

nafananisha hii na yule mkuu wa majeshi aliyeaibisha jeshi aligombea na kubwagwa katika hatua za awali

another disappointing news today!
 
Huyu bwana akikaa pembeni ataheshimika zaidi. Wamuangalie Desmond Tutu anavyoheshimika. Ukienda mbali zaidi utaona namna vyama vya upinzani vina kazi maana kwenye nyumba za ibada CCM inahubiriwa. Labda waraka unaweza kuwa mwanzo wa mabadiliko otherwise inawezekana kuwepo na uhusiano kati ya uongozi wa dini na uanachama wa chama cha siasa. Ikifika hapo waumini nao watachagua nyumba za ibada kutokana na kiongozi wa nyumba hiyo kuwa mwanachama wa chama fulani. Maana unaona Lwakatare yupo bungeni, Mwamasika etc. What next Mufti au kardinali?
 
Inasikitisha kuona watanzania wengi wanafikiri bila kuingia kwenye siasa hawawezi kuishi, wanataka pesa za bure za wananchi kwani hata bunge la tanzania ni kama hakuna bunge.
 
Ndiye aliwaambia watanzania kuwa JK ni chaguo la Mungu. Kumbe alikuwa anajiandalia njia ya kurudi kwenye siasa.
 
ukistaafu unatafuta madaraka sehemu nyingine lol.
sasa taifa la vijana ndo litakuwa la kesho kila siku
 
politics ya Tz imekuwa shamba la bibi!
Komaa Askofu unaweza kutoka kimtindo ila usije ukawa kimya kama mama rwakatale
 
Huyu Askofu alishawahi kutembea na mke wa mtu,pale Dom,miaka ya 1990s,akasababisha ndoa iharibike.Kwa hiyo asijifanye kuwa yeye ni msafi.Mme mtu ilibidi amuachie 'askofu'.Ndio hypocricy ambayo tunayo.
 
..amestaafu Uaskofu.

..mwacheni ajaribu kwani ni haki yake.
 
Mimi sipendezwi sana na viongozi wa dini kugombea nafasi za kisiasa. Naona kama ni a very big contradiction. Sijui but my gut feeling tells me huyu nae ni wale wale tu.
 
..amestaafu Uaskofu.

..mwacheni ajaribu kwani ni haki yake.
Well said
Katiba inaruhusu kila mwananchi kuchagua na kuchaguliwa

Ni mtazamo tu ambao watu wanao, kuhusu viongozi wa dini nafikiri ni high time waruhusiwe wote masheikh, wachangaji, walimu wa madrasa (kama mimi) tuingie huko labda tutawasaidia hawa wasio na dini hasa uadilifu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…