Sipendi kuchangia thread kama hizi lakini kwa hili la Mwingira itabidi. Hii si mara ya kwanza Mwingira anaingia kwenye migogoro na waumini wake juu ya viwanja. Huyu ni tapeli anatumia imani za watu vibaya kuwatapeli ardhi, na anapaswa ashitakiwe kwa wizi wa kuaminiwa.
Wale walio tasnia ya sheria watakumbuka Mwingira alifanikiwa kumuingiza Advocate Hubert Mbuya (alishakufa) kwenye kanisa lake na akawa rafiki wa kanisa. Alipojua Mbuya ana kiwanja kikubwa pale Kawe akamshawishi akitoe "kwa ajili ya Mungu". Mbuya akakubali kutoa kiwanja chake bure na kumkabidhi Mwingira kitumike kwa ajili ya kazi za Mungu.
Sasa baadae ilikuja kujulikana kuwa Mwingira alikuwa anajifanya yuko karibu na Mbuya kumbe alikuwa anatembea na mke wa Mbuya. Mbuya alipopata taarifa alidai Mwingira amrudishie kiwanja chake kwa sababu yeye sio mtumishi wa kweli wa Mungu, ni tapeli. Mwingira aligoma kurudisha kiwanja.
Mbuya alimshitaki Mwingira mahakamani lakini alishindwa ile kesi, kwa sababu alipomkabidhi kiwanja hakuna mahali makabidhiano yalisema nikitembea na mke wako itabidi nirudishe kiwanja. Mahakama iliona kuwa suala la Mwingira kutembea na mke wa Mbuya halikuhusiana na mkataba wa Mbuya kutoa kiwanja chake.
Mwingira alikuwa mjanja wa kukabidhiana kiwanja kwa maandishi, naona ndili alilowafanyi ahawa watu huko. Ni tapeli huyu anapaswa kukamatwa na kuwekwa ndani