Je, hawo wananchi wenye akili ma vi kama za CCM ikiwa wao ndio wamevamia viwanja vya Mwingira wakajenga kwa nguvu ulitaka awachekee?Watumishi wa Mungu wanagombania pesa na mali, mchungaji anagombania ardhi ya wananchi. Mwingira wa efatha anatia aibu watumishi
Hapo unakuta kuna wamama wanaamini mwingira ndio mlezi wao wa kiroho wa kuwafikisha mbinguni, huku mchungaji mwenyewe anavunja nyumba za wananchi ili apate ardhi
View attachment 3010162
Mkuu umeongea ukweli tupu. Sasa kama wananchi wamevamia maeneo yake alitaka awachekee ili iweje?Mkuu mbona unatoa taarifa huku unaonekana Una chuki na upande mmoja.....hayo makanisa si yanajengwa juu ya ardhi..... kwanini wasiwe au wasimiliki ardhi........
Hata yeye ana haki ya kumiliki ardhi kulingana na sheria na utaratibu wa nchi.......
Jitahidi unapotoa habari ujitenge na mihemko unaweza ukaonekana unapiga majungu badala ya kuleta habari........
Hakika ndugu......Mkuu umeongea ukweli tupu. Sasa kama wananchi wamevamia maeneo yake alitaka awachekee ili iweje?
Hapo sidhani kama kuna kesi ila ukute wananchi ndiyo dizaini ya wale wanaouza ardhi na kutakiwa kuhama ila wanajibu, ngoja tunajenga huko makazi mapya.
Mfanyabiashara muwekezaji ndg mchungaji anakuja kutaka kuwekeza kwenye eneo lake, anaonekana mbaya.
Note this na subiri jibu siku si nyingi.
Sipendi kuchangia thread kama hizi lakini kwa hili la Mwingira itabidi. Hii si mara ya kwanza Mwingira anaingia kwenye migogoro na waumini wake juu ya viwanja. Huyu ni tapeli anatumia imani za watu vibaya kuwatapeli ardhi, na anapaswa ashitakiwe kwa wizi wa kuaminiwa.
Wale walio tasnia ya sheria watakumbuka Mwingira alifanikiwa kumuingiza Advocate Hubert Mbuya (alishakufa) kwenye kanisa lake na akawa rafiki wa kanisa. Alipojua Mbuya ana kiwanja kikubwa pale Kawe akamshawishi akitoe "kwa ajili ya Mungu". Mbuya akakubali kutoa kiwanja chake bure na kumkabidhi Mwingira kitumike kwa ajili ya kazi za Mungu.
Sasa baadae ilikuja kujulikana kuwa Mwingira alikuwa anajifanya yuko karibu na Mbuya kumbe alikuwa anatembea na mke wa Mbuya. Mbuya alipopata taarifa alidai Mwingira amrudishie kiwanja chake kwa sababu yeye sio mtumishi wa kweli wa Mungu, ni tapeli. Mwingira aligoma kurudisha kiwanja.
Mbuya alimshitaki Mwingira mahakamani lakini alishindwa ile kesi, kwa sababu alipomkabidhi kiwanja hakuna mahali makabidhiano yalisema nikitembea na mke wako itabidi nirudishe kiwanja. Mahakama iliona kuwa suala la Mwingira kutembea na mke wa Mbuya halikuhusiana na mkataba wa Mbuya kutoa kiwanja chake.
Mwingira alikuwa mjanja wa kukabidhiana kiwanja kwa maandishi, naona ndili alilowafanyi ahawa watu huko. Ni tapeli huyu anapaswa kukamatwa na kuwekwa ndani
Nakazia hoja.Mkuu mbona unatoa taarifa huku unaonekana Una chuki na upande mmoja.....hayo makanisa si yanajengwa juu ya ardhi..... kwanini wasiwe au wasimiliki ardhi........
Hata yeye ana haki ya kumiliki ardhi kulingana na sheria na utaratibu wa nchi.......
Jitahidi unapotoa habari ujitenge na mihemko unaweza ukaonekana unapiga majungu badala ya kuleta habari........
Sidhani kama iko hivyo kama inavyoripotiwa. Isije kuwa watu wanamwuzia ardhi halafu baadaye wanarudi kinyume-nyume kutaka kuitumia hiyo ardhi ilhali walishalamba asali.Nilisoma mahali Huko Rukwa nako amefunguliwa kesi ya kupora ardhi ya watu.
We jamaa unapenda sana ugomvi sasa umemwita huyo Mgerasi Ili agundue nini huijui nickname yake ya Trouble maker?Maghayo Stress Challenger Njoo uone
Fuatilia vizuri kuna maeneo mengi ana migogoro ya ardhi, nadhani anaipata kwa ujanja ujanja.Sidhani kama iko hivyo kama inavyoripotiwa. Isije kuwa watu wanamwuzia ardhi halafu baadaye wanarudi kinyume-nyume kutaka kuitumia hiyo ardhi ilhali walishalamba asali.