Askofu Mwingira avunja nyumba za wananchi Handeni. Mkuu wa wilaya aamuru Askofu akamatwe

Hili uliloelezea limenichekesha japo mhusika mmoja ni marehemu sasa. Kulingana na maelezo yako kosa lilikuwa ni la marehemu. Bora angechukuwa njia za kimafia kukabiliana naye na siyo mahakama. BTW hawa wanaojiita viongozi wa dini wengi ni matapeli na lakini utapeli wao hauwezi kutufanya kuhukumu hii case yake hapa. Unaweza kukuta alifuata njia halali kupata eneo. BTW Tanzania hii migogoro ya ardhi ni ya kujitakia kwani inazuilika kama tutabadilisha mfumo wa umiliki na ununuzi wa ardhi. Najua CCM hawataki ili watu kama kina Makonda waweze kuwaghilibu wananchi kuwa ni wachapakazi wakati ni kama wanajaza wanachota maji baharini wakitarajia kuikausha.
 
Unasema kweli. Watu walimshauri sana Advocate Mbuya asitoe kile kiwanja kwa Mwingira, nasikia hata baba yake, lakini hakusikia. Kwa hiyo majuto yakawa mjukuu kwake. Na ilikuwa so embarrassing kwa advocate mtu mzima kama yeye kuelezea mahakamani jinsi Mwingira alivyokuwa akitembea na mke wake huku akijifanya ni mlezi wa kiroho wa familia yake. Nilitegemea baada ya hapo, Mwingira angebaki na kiwanja lakini angepoteza waumini wake wote, maana Mwingira hakupinga dai la kutembea na mke wa Mbuya, bali alisimamia kwenye upande kuwa hili halibatilishi makubaliano ya kukabidhiwa kiwanja na Mbuya.

Mbaya zaidi mke wa Mbuya alidai Mwingira alimuambukiza ugonjwa wa zinaa uliomchukua miaka mitatu bila kupona, ndipo akapata maono atubu kwa mumewe ili apone. Naona ilikuwa remorse tu inamsumbua.

Pamoja na yote hayo, bado wajinga wengi waliendelea kumfuata Mwingira kama mchungaji wao. Kuna watu akili zao zinahitaji sabuni, tena ile inayobabua kabisa!
 
Kweli hata mimi nilisikia,jamaa akiona kuna ardhi sehemu akiitamani tu lazima afanye yake aichukue
Huyu ni tapeli, lakini watu bado wanamfuata. Amekuwa kama chama cha siasa, ambapo mara nyingi hata kiwe na ujinga gani kuna watu watakishabikia tu huwaambii kitu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…