Askofu Nkwande: Bungeni sio mahali pa kufanya mambo ya mzaha au kuongelea utoaji mimba na mapenzi ya jinsia moja

Askofu Nkwande: Bungeni sio mahali pa kufanya mambo ya mzaha au kuongelea utoaji mimba na mapenzi ya jinsia moja

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Askofu mkuu wa Jimbo Kuu la Mwanza, Renatus Nkwande amesema bungeni ni mahali patakatifu na si pa kwenda kufanya mzaha na kuzungumza kuhusu uzazi wa mpango, utoaji mimba au mapenzi ya jinsia moja.

Ameeleza hayo Ijumaa Machi 26, 2021 katika ibada ya mazishi ya Rais wa Awamu ya Tano wa Tanzania Hayati John Magufuli inayofanyika katika uwnaja wa Magufuli wilayani Chato Mkoa wa Geita.

“Bungeni ni mahali patakatifu si mahali pa kwenda kufanya mizaha unakwenda kuanza kuzungumza kuhusu mambo ya uzazi wa mpango, utoaji mimba au mapenzi ya jinsia moja.”

“Hao wenzetu ambao walitumia hizo njia za uzazi wa mpango wameathirika vizazi kwa vizazi leo hii wanatafuta watoto hawapati licha ya kuambiwa ukizaa mmoja utamtunza ukiongeza wa pili tutamtunza bado mambo yamekuwa magumu,” amesema Askofu Nkwande.


Chanzo: Mwananchi
 
Huyu asikofu aliishawahi kumpa mwanamke mimba, je anajua lolote kuhusu kuzaa na kulea ,je anafikiri usipoyajadili hayo hizo sheria za kuyasimamia utazitunga vipi ? Huyu asikofu aendelee na mambo yake ya dini haya mambo ya bunge atuachie sisi na wabunge wetu.
 
Nilisikiliza hotuba yake, amewawahi wanaharakati kwani siku zote wanatetea wanachoambiwa na wafadhili wao na sio chenye manufaa
 
Hili la uzazi wa mpango alitakiwa afafanue ni njia zipi si nzuri kwa afya ya kimwili na kiroho kwa mwanadamu au ndio kusema Baba Askofu hajui kama kuna njia za kimaumbile ambazo ni salama kimwili na kiroho?Alitakiwa awasiliane na jumuiya ya wataalamu wa afya wa kanisa kabla ya kuliongelea hili.
 
Back
Top Bottom