Pre GE2025 Askofu shoo ni kama amepoteza mwelekeo, hajui anataka nini

Pre GE2025 Askofu shoo ni kama amepoteza mwelekeo, hajui anataka nini

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

kingito

Member
Joined
Sep 10, 2024
Posts
10
Reaction score
3
Salaam wanaforum wenzangu

Wiki chache zilizopita tulishuhudia askofu Shoo akimnadi Rais Samia kuwa aongezewe miaka mitano tena huku akisema huyu mama amefanya mambo makubwa sana katika kipind hiki alichokaa madarakani

Soma pia:
Alithubutu kusema kuwa Rais Samia ameletwa na Mungu katika kipindi hii. Jambo hili zilizua gumzo sana mtandoni

Leo katika jukwaa la viongozi wa dini Askofu shoo amenukuliwa akisema kuwa mambo ya kisiasa yanayoendelea nchini ni kama vile yamataka kujirudia yale ya mwaka 2019/2029

Soma Pia:
Amedai zaidi kuwa Tanzania kwa sasa inahitaji katiba mpya yenye tume huru ya uchaguzi kuelekea uchaguzi wa mwakani

Binafsi ni kama huyu Askofu anag'ata na kupuliza. Ukimfuatilia kwa makini huelewi ana msimamo gan katika siasa za tanzania.

Binafsi namshauri akae kimya tuu hajui anataka nini!

Anatuchanganya sana.
 
Labda hizo hela za majini zimeanza kumchanganya akili.
 
Back
Top Bottom