Aslay na Mario nawakubali sana, pamoja na ustaa wao wanaishi maisha ya kawaida sana

Aslay na Mario nawakubali sana, pamoja na ustaa wao wanaishi maisha ya kawaida sana

kidochi og

Member
Joined
May 27, 2020
Posts
45
Reaction score
74
Ni wasanii wa bongo freva ambao ukiachilia mbali mond, kiba, konde. Wana wafuasi wengi Sana kwenye mitandao ya kijamii.

Hiyo inaashilia ukubwa wao na ni kiashirio cha kwamba wanakubalika sana mtaani.

Pia ni wasanii ambao hawategemei kiki au promo yeyote ile ili wasogeze muziki wao.

Kutokana na ubora wa nyimbo zao zinajisogeza zenyewe.

Ni wasanii nawakubali sana. Pamoja na ustaa wao wanaishi maisha ya kawaida sana.

Aslay_nibebe,kwatu, nichombeze
Mario_inatosha,Raha, chibonge

Unamkubali Nani zaidi??!!

FB_IMG_15988818555894809.jpg
FB_IMG_15988819118786920.jpg

"We kidawa kwa nini unautesa moyo kidawa......?" hii nyimbo hatari,Mario mzuri ila bado hajafikia level za Aslay.

Sizani kama kuna msanii alishawahi kutoa hiti zaidi ya 14 ndani ya mwaka mmoja zaidi ya Aslay.
 
Aslay yuko juu sana ila hawa majamaa washawahi kweli wimbo wa amshaamsha kama za club ?hii style yao kila wimbo wanalia inakera
 
Aslay yuko juu sana ila hawa majamaa washawahi kweli wimbo wa amshaamsha kama za club ?hii style yao kila wimbo wanalia inakera
Marioo ana bangers kadhaa za moto

✓Tikisa
✓Anyinya
✓Wauwe
 
"We kidawa kwa nini unautesa moyo kidawa......?" hii nyimbo hatari,Mario mzuri ila bado hajafikia level za Aslay.

Sizani kama kuna msanii alishawahi kutoa hiti zaidi ya 14 ndani ya mwaka mmoja zaidi ya Aslay.
Binafsi namkubali Sana Mario kidogo huwa anabadilikabadilika compare na aslay
 
Kwenye ndinga langu namsikilizaga sana Marioo. Aslay nyimbo za kwenye daladala, na kulialia maisha every day.
 
Back
Top Bottom